Biriani Ya Kuku Wa Kuoka (Baked) Kwa Sosi Ya Zaafarani Na Rosi

 

Biriani Ya Kuku Wa Kuoka (Baked) Kwa Sosi Ya Zaafarani Na Rosi

 

 

 

Vipimo

 

Mchele ulionyooka (basmati/pishori) – Vikombe 3

Kuku – 1

Vitunguu – 5

Nyanya 3

Majani ya bay (bay leaves) kiasi mawili

Bizari ya biriani – kijiko cha supu.

Hiliki nzima chembe 5

Bizari ya manjano (haldi/turmeric)  1 kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga – kijiko 1 cha chai

Chumvi kiasi

Mafuta kiasi

Zaafarani – kijiko 1 kimoja

Arki (rose water)

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

 1. Roweka mchele kiasi ya nusu saa au saa moja kulingana na aina ya mchele.
 2. Muoshe kuku mkatekate vipande saizi upendayo. Usimtoe ngozi.
 3. Mchepushe kuku kwa viungo upendavyo kama chumvi, siki, tangawizi mbichi na thomu na ndimu. Kisha mwache muda kiasi.
 4. Muoke (bake) kuku katika oveni mpaka awive. Mtoe mweke kando. Atakuwa ametoa supu yake kiasi, imimine katika kibakuli.
 5. Weka mafuta kiasi, tia bay leaves, kaanga kidogo kisha tia vitunguu ukaange mpaka vigeuke rangi iwe ya hudhurungi (golden borwn).
 6. Katakata nyanya vipande vikubwa kiasi na ukaange kidogo. Tia bizari zote.
 7. Mimina supu kiasi iliyotoka katika kumuoka kuku, kiasi ya nusu kikombe. Changanya vizuri.
 8. Mtie kuku umchganye vizuri na masala. Weka kando masala.
 9. Chemsha mchele ukishaiva nusu kiini mwaga maji.
 10. Changanya zaafarani na maji ya rosy kisha nyunyizia katika mchele pale unapomimina mchele juu ya sosi ya biriani.
 11. Funika uweke katika moto mdogo mdogo mpaka mchele uive.
 12. Pakua katika sahani masala yakiwa juu ya wali.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share