Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku (Chicken Breast) Wa Kukausha

Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku

  

Vipimo vya Wali:

Mchele  -   3 vikombe

*Maji ya kupikia  -  5 vikombe 

*Kidonge cha supu -  1

Samli - 2 vijiko vya supu

Chumvi  kiasi

Hiliki  - 3 chembe

Bay leaf -    1                                             

 

Vipimo Vya Kuku

Kidari (chicken breast)  - 1Kilo

Kitunguu -  1

Tangawizi mbichi -   ½ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) -  7 chembe

Pilipili mbichi  -   3

Ndimu  - 2

Pilipilimanga -  1 kijiko cha chai

Mdalasini  - ½ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga  - 1 kijiko cha chai

Maji  -   ¼ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Wali:

  1. Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
  2. Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
  3. Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
  4. *Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
  5. *Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

  1. Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
  2. Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
  3. Chuna tangawizi mbichi  tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
  4. Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka  epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)
Share