Swalah Mwenye Kusafiri Mara Kwa Mara

 

SWALI

Nina ndugu yangu miaka 20 mtoto wa kiume.  Sisi ni wa Oman lakini yeye anakwenda mara kwa mara Tanzani.  Swari lenyewe ni kwamba yeye anasema ansali safari hapa na Tanzania je hiyo ni sawa?  Mimi nimemwambia yeye ni muomani mafuludhi asali watani hapa akasema la kwasababu mara nying anakaa miezi mitatu hapa na anakwenda Tanzania miezi mitatu kwa hiyo anasali safari siku zote. Naomba musaada wenu.

 

 


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako ambalo ni muhimu kwetu kuelewa misingi ya kukusuru (kuswali Swalah ya safari kwa kupunguza baadhi ya Swalah hasa zile za rakaa nne na kuwa mbili). Moja ya msingi ni kuwa huwezi kuswali Swalah ya safari sehemu ambayo wewe ni mkazi hata kwa nusu siku

Kwa mfano nduguyo ni mkazi wa Oman, hivyo anapofika tu katika mji anaoishi kwa mfano Muscat basi anatakiwa aswali Swalah kamili hata kama atakaa nusu siku pekee na kuwahi baadhi ya Swalah. Pindi anapokwenda safari ya nje ya mji wake na akawa ashapanga tayari kuwa atakaa kwa mfano hiyo miezi mitatu katika mji mmoja wa Tanzania (mfano Tanga) inabidi aswali Swalah kamili kwani huwa anajua siku anazokaa kumfanya awe na utulivu.

Maelezo zaidi kuhusu Swalah ya Safari yapo hapa

 

Swalah Ya Safari Ya Mtu Anayeishi Katika Nchi Muda Mrefu

 

 

Lakini hii haina maana kama wewe umetoka nchi fulani na ukaenda nchi nyingine kimaisha na ukatamakani katika nchi hiyo kama ambavyo wengi waliokwenda Ulaya na Marekani kutafuta maisha na kisha wakatamakani wakapata makazi ya kudumu na hata kupata vizazi vyao huko, basi ni bora na awlaa kuswali kikamilifu kuliko kufupisha. Na haipendezi mtu kujidanganya nafsi yake kuwa si kwake hapo na si nchi yake na hali keshakaa miaka na hadi kupata watoto na bado hana dalili ya kuondoka na labda hata moyoni mwake anajua kabisa kuwa haondoki! Basi tunawanasihi watu wasiitumie sheria hiyo kuwa wavivu katika Ibaada.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share