05-Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam: Kutokuua Nafsi Aliyoharamisha Allaah Ila Kwa Haki

 

Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam  

 

05-Kutokuua Nafsi Aliyoharamisha Allaah, Ila Kwa Haki

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ

Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). [Al-An’aam: 151] 

 

Adhabu kali mno zifuatazo Amezitahadharisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa atakayemuua Muislamu bila ya haki:

 

 

1-Kuingizwa motoni na kudumu milele.

 

2-Kughadhibiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

3-Kulaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

4-Kuandaliwa adhabu kubwa.

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾

Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu. [An-Nisaa: 93]

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya pia katika Hadiyth:

 

عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ  إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)).  رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ    

Kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alisema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Damu ya Muislamu haipasi kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi muolewa (Mtu  mzima aliyeoa au aliyeolewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anayeacha Dini  na akajifarikisha na  jama’ah   (amejitenga na watu wa Dini yake)) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hata kuua wasio Waislamu pasi na haki pia imeharamsihwa. Mwenye kufanya hivyo hataisikia harufu ya Pepo kwa dalili:

 

 عَنْ عَبْد اللَّه بْن عُمَر عَنْ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرْفُوعًا ((مَنْ قَتْل مُعَاهَدًا لَمْ يُرَحْ رَائِحَة الْجَنَّة وَإِنَّ رِيحهَا لَيُوجَد مِنْ مَسِيرَة أَرْبَعِينَ عَامًا))

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar ambaye amesema: ((Yeyote aliyeua mtu ambaye alikuwa katika ahadi na kuhifadhiwa na Waislamu, hatasikia harufu ya Jannah japokuwa harufu yake inasikika umbali wa miaka arubaini)) [Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة عَنْ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ قَتَلَ مُعَاهَدًا لَهُ ذِمَّة اللَّه وَذِمَّة رَسُوله فَقَدْ أَخْفَرَ بِذِمَّةِ اللَّه فَلَا يُرَحْ رَائِحَة الْجَنَّة وَإِنَّ رِيحهَا لَيُوجَد مِنْ مَسِيرَة سَبْعِينَ خَرِيفًا))

 

Na kutoka wa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote aliyeua mtu akiwa katika ahadi yya kuhifadhiwa na Waislamu, na ambaye ananufaika na dhamana ya Allaah na Rasuli Wake, atakuwa ameharibu dhamana ya Allaah, (kwake). Hatasikia harufu ya Jannah japokuwa harufu yake inasikika kutoka umbali wa miaka sabini)) [al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share