08-Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam: Kushuhudia Na Kufanya Uadilifu Japokuwa Dhidi Ya Jamaa Wa Karibu

 

Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam  

 

08- Kushuhudia Na Kufanya Uadilifu Japokuwa Dhidi Ya Jamaa Wa Karibu

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa):

 

وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ

Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. [Al-An’aam: 152]

 

Ni kusema ukweli na kuweka uadilifu katika kushuhudia jambo dhidi ya mtu binafsi au watu walio na uhusiano wa karibu.   Uadilifu huu unaweza kuwa katika kutoa hukmu, au kushuhudia jambo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kauli Yake nyengine:  

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾

  Enyi walioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate hawaa mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkikanusha basi hakika Allaah daima kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa: 135]

 

 

 Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

Kusema yaliyo haki na kufanya uadilifu inapaswa hata kwa mtu ambaye una chuki na uadui naye, madamu tu yuko katika haki basi lazima useme ukweli.   Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

Enyi walioamini!  Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo.  [Al-Maaidah: 8]

 

Uadilifu unatakiwa pia hata katika kugawa vitu baina ya watu wenye haki navyo: 

 

عَنْ النُّعْمَان بْن بَشِير أَنَّهُ قَالَ : نَحَلَنِي أَبِي نُحْلًا فَقَالَتْ أُمِّي عَمْرَة بِنْتُ رَوَاحَةَ : لَا أَرْضَى حَتَّى تُشْهِد عَلَيْهِ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَهُ لِيُشْهِدهُ عَلَى صَدَقَتِي فَقَالَ  ((أَكُلَّ وَلَدِك نَحَلْت مِثْلَهُ ؟))  قَالَ لَا قَالَ:  ((اِتَّقُوا اللَّه وَاعْدِلُوا فِي أَوْلَادكُمْ)) وَقَالَ – ((إِنِّي لَا أَشْهَد عَلَى جَوْر))  قَالَ فَرَجَعَ أَبِي فَرَدَّ تِلْكَ الصَّدَقَة" البخاري و مسلم

Kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr ambaye amesema: “Baba yangu alinipa zawadi lakini mama yangu ‘Amrah bint Rawaahah hakuridhikia hadi ashuhudie Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baba yangu akamwendea, akamtaka ashuhudie kunipa kwake zawadi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: ((Je, umewapa hivyo hivyo kwa watoto wako wengine?)) Akajibu. Hapana. Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mche Allaah, na adilisha [timiza haki] kwa watoto wako)) Akasema: ((Mimi sishuhudii dhidi ya dhulma)) Kisha baba yangu akarudisha zawadi yake: [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share