027-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Kuadhimisha Mambo Matukufu Ya Waislamu, Kubainisha Haki, Kuwasikitia Na Kuwahurumia

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تعظيم حرمات المسلمين وبيان حقوقهم والشفقة عليهم ورحمتهم

27 – Mlango Kuadhimisha Mambo Matukufu Ya Waislamu, Kubainisha Haki, Kuwasikitia Na Kuwahurumia

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ﴿٣٠﴾

Na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Rabb wake. [Al-Hajj: 30]

 

وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 32]

 

وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾

 Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia). [Al-Hijr: 88]

 

مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ﴿٣٢﴾

Atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. [Al-Maaidah: 32]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((المُؤْمِنُ للْمُؤْمِنِ كَالبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا)) وشبَّكَ بَيْنَ أصَابِعِهِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muumini kwa Muumini ni mfano wa jengo, sehemu moja inatilia nguvu sehemu nyingine.” Na akaviunganisha vidole vyake. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ مَرَّ في شَيْءٍ مِنْ مَسَاجِدِنا، أَوْ أَسْوَاقِنَا، وَمَعَهُ نَبْلٌ فَلْيُمْسِكْ، أَوْ لِيَقْبِضْ عَلَى نِصَالِهَا بكَفّه؛ أنْ يُصِيبَ أحَدًا مِنَ المُسْلِمِينَ مِنْهَا بِشَيْء)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwake Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Anayepita Misikitini au masokoni mwetu na ilhali ana mshale, basi auzuwie au akishike chemba chake kwa mkono wake, asije akamdunga nao yeyote katika Waislamu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 3

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلُ المُؤْمِنينَ في تَوَادِّهِمْ وتَرَاحُمهمْ وَتَعَاطُفِهمْ، مَثَلُ الجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الجَسَدِ بِالسَّهَرِ والحُمَّى)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusaidiana kwao, ni mfano wa mwili, kiungo kimoja kikiumwa basi mwili mzima hukesha kwa homa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَبَّلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم الحَسَنَ بْنَ عَليٍّ رضي الله عنهما، وَعِنْدَهُ الأَقْرَعُ بْنُ حَابِس، فَقَالَ الأقْرَعُ: إن لِي عَشرَةً مِنَ الوَلَدِ مَا قَبَّلْتُ مِنْهُمْ أحَدًا. فَنَظَرَ إِلَيْهِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((مَنْ لا يَرْحَمْ لا يُرْحَمْ!)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuna wakati mmoja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimbusu mjukuu wake Al-Hasan bin ‘Ally (Radhwiya Allaahu 'anhu) mbele ya Al-Aqra akasema: “Hakika mimi nina watoto kumi sijambusu yeyote miongoni mwao.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alimtazama, akasema: “Yeyote asiye na huruma (kwa wenziwe) basi hahurumiwi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: قَدِمَ نَاسٌ مِنَ الأعْرَابِ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فقالوا: أتُقَبِّلُونَ صِبْيَانَكُمْ؟ فَقَالَ: ((نَعَمْ)) قالوا: لَكِنَّا والله مَا نُقَبِّلُ! فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((أَوَ أَمْلِك إنْ كَانَ اللهُ نَزَعَ مِنْ قُلُوبِكُم الرَّحْمَةَ))!. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

في هذا الحديث: الشفقة على الأولاد، وتقبيلهم ورحمتهم.

Imepokewa na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) aliyesema: Mabedui walikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), wakasema: “Je, mnawabusu watoto wenu?” Akasema: “Ndio.” Wakasema: “Lakini sisi Wa-Allaahi hatuwabusu.” Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akasema: “Je, naweza kuwamiliki ikiwa Allaah Ameondosha nyoyoni mwenu rehma (huruma).” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 6

وعن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ لا يَرْحَم النَّاسَ لا يَرْحَمْهُ الله)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na Jariyr bin ‘Abdillaahi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Asiye wahurumia watu, Allaah Hamrehemu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِذَا صَلَّى أحَدُكُمْ للنَّاسِ فَلْيُخَفِّفْ، فَإن فيهِم الضَّعِيفَ وَالسَّقِيمَ وَالكَبيرَ، وَإِذَا صَلَّى أحَدُكُمْ لِنَفْسِهِ فَلْيُطَوِّل مَا شَاءَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Anaposwalisha watu mmoja wenu basi akhafifishe, kwani wapo miongoni mwao wanyonge, wagonjwa na wazee. Na anaposwali mmoja wenu peke yake, arefushe anavyotaka.” Na katika riwayah yengine: “Wenye haja.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: إنْ كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَيَدَعُ العَمَلَ، وَهُوَ يُحبُّ أنْ يَعْمَلَ بِهِ؛ خَشْيَةَ أنْ يَعمَلَ بِهِ النَّاسُ فَيُفْرَضَ علَيْهِمْ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwake ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) mara nyengine alikuwa akiacha 'amali naye anapenda kuitekeleza kwa kuogopea wasije wakaifanya hivyo kufaradhishwa kwao. [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 9

وَعَنْهَا رضي الله عنها قَالَتْ: نَهَاهُمُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عنِ الوِصَال رَحمَةً لَهُمْ، فَقَالُوا: إنَّكَ تُوَاصِلُ؟ قَالَ: ((إنّي لَسْتُ كَهَيْئَتِكُمْ، إنِّي أبيتُ يُطْعمُني رَبِّي وَيَسقِيني)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Amesema ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) aliwakataza Wiswaal kwa kuwahurumia wao. Wakasema: “Hakika wewe unaunganisha?” Akasema: “Hakika mimi si kama mmoja wenu. Hakika mimi ninalishwa na kunyweshwa na Mola wangu usiku.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي قَتادةَ الحارثِ بن رِبعِي رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنِّي لأَقُومُ إِلَى الصَّلاة، وَأُرِيدُ أنْ أُطَوِّلَ فِيهَا، فَأسْمَع بُكَاءَ الصَّبيِّ فَأَتَجَوَّزَ في صَلاتي كَرَاهية أنْ أشُقَّ عَلَى أُمِّهِ)). رواه البخاري.

Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Haarith Ar-Ri’biy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Kwa hakika mimi husimama katika Swalah na nikataka kuirefusha, basi huwa nikisikia kilio cha mtoto, hapo naifupisha Swalah yangu kwa kuchelea nisije nikampa uzito mama yake.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 11

وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى صَلاةَ الصُّبْحِ فَهُوَ في ذِمَّةِ الله فَلا يَطْلُبَنَّكُمُ الله مِنْ ذِمَّته بشَيءٍ، فَإنَّهُ مَنْ يَطْلُبْهُ منْ ذمَّته بشَيءٍ يُدْركْهُ، ثُمَّ يَكُبُّهُ عَلَى وَجْهِهِ في نَارِ جَهَنَّمَ)). رواه مسلم.

Kutoka kwa Jundub bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mwenye kuswali Swalaah ya Al-Fajr yuko katika dhima ya Allaah (amani na ahadi Yake). Hivyo, usijiweke katika hali ambayo utakuja laumiwa na Allaah kwa kuvunja ahadi Yake. Hakika mwenye kufanyiwa hesabu kwa kufanya khiyana ulinzi wa Allaah, Allaah Atampatiliza, na kisha kumuingiza kwa uso wake moto wa Jahannam.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 12

وعن ابن عمر رضي الله عنهما أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((المُسْلِمُ أَخُو المُسْلِم، لا يَظْلِمهُ، وَلا يُسْلمُهُ. مَنْ كَانَ في حَاجَة أخيه، كَانَ اللهُ في حَاجَته، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِم كُرْبَةً، فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ بها كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَومِ القِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللهُ يَومَ القِيامَةِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Mwenye kumtekelezea haja nduguye, Allaah Atamtekelezea haja yake. Mwenye kumondolea Muislamu dhiki, Allaah humondolea dhiki miongoni mwa dhiki Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمُ، لا يَخُونُهُ، وَلا يَكْذِبُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ، كُلُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِم حَرَامٌ عِرْضُهُ وَمَالهُ وَدَمُهُ، التَّقْوى هاهُنَا، بحَسْب امْرئٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحْقِرَ أخَاهُ المُسْلِم)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن)).

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Muislamu mwengine, hamfanyii khiyana wala hamdanganyi wala haachi kumnusuru. Kila Muislamu mwenziwe ni haramu cheo (heshima) chake, mali yake na damu yake. Taqwah ipo hapa, inatosha kwa mtu kuwa katika shari kumchukia nduguye Muislamu.” [At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 14

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تَحَاسَدُوا، وَلا تَنَاجَشُوا، وَلا تَبَاغَضُوا، وَلا تَدَابَرُوا، وَلا يَبعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْع بَعْض، وَكُونُوا عِبَادَ الله إخْوَانًا، المُسْلِمُ أخُو المُسْلم: لا يَظْلِمُهُ، وَلا يَحْقِرُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ، التَّقْوَى هاهُنَا- ويشير إِلَى صدره ثلاث مرات-- بحَسْب امْرئٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحقِرَ أخَاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلم عَلَى المُسْلم حَرَامٌ، دَمُهُ ومَالُهُ وعرْضُهُ)). رواه مسلم.

Kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Msihusudiane, wala msiongezeane bei (katika biashara), wala msitukanane, wala msipeane nyongo (msikatane), wala baadhi yenu wasiuze juu ya wageni; na kuweni nyote ni waja wa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa), ndugu moja. Muislamu ni ndugu ya Muislamu; hamdhulumu wala hamdharau, wala haachi kumnusuru. Uchaji Allaah uko hapa – akaashiria mara tatu kifuani mwake – yatosha mtu kutenda sharia atakapomdharau nduguye Muislamu. Kila Muislamu juu ya Muislamu mwenziwe ni haramu: damu yake, mali yake na heshima yake.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

وعن أنس رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لا يُؤمِنُ أحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لأخِيهِ مَا يُحِبُّ لنَفْسِهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Haamini mmoja wenu mpaka ampende nduguye kwa analolipendelea nafsi yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 16

وعنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((انْصُرْ أخَاكَ ظَالمًا أَوْ مَظْلُومًا)) فَقَالَ رجل: يَا رَسُول اللهِ، أنْصُرُهُ إِذَا كَانَ مَظْلُومًا، أرَأيْتَ إنْ كَانَ ظَالِمًا كَيْفَ أنْصُرُهُ؟ قَالَ: ((تحْجُزُهُ- أَوْ تمْنَعُهُ- مِنَ الظُلْمِ فَإِنَّ ذلِكَ نَصرُهُ)). رواه البخاري.

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mnusuru nduguyo akiwa amedhulumu au amedhulumia.” Mtu mmoja akauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Nitamnusuru akiwa amedhulumiwa, nieleze nitamnusuru vipi akiwa amedhulumu?” Akasema: “Mzuilie asidhulumu, kufanya hivyo ndiko kumnusuru.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 17

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((حَقُّ المُسْلِم عَلَى المُسْلِم خَمْسٌ: رَدُّ السَّلامِ، وَعِيَادَةُ المَريض، وَاتِّبَاعُ الجَنَائِزِ، وَإجَابَةُ الدَّعْوَة، وتَشْميتُ العَاطِسِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Haki ya Muislamu kwa Muislamu mwenziwe ni tano: Kurudisha salamu, kumzuru mgonjwa, kumfuata jeneza, kuitikia mwaliko na kumwombea du’aa aliyepiga chafya (aliyechumua).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah ya Muslim: “Haki za Muislamu ni sita: Unapokutana naye umsalimie, anapokualika umwitikie, akitaka nasaha mnasihi, anapochemua na akamuhimidi Allaah muombee du’aa, akiwa mgonjwa mzuru na anapokufa fuata (jeneza lake).”

 

 

Hadiyth – 18

وعن أَبي عُمَارة البراءِ بن عازب رضي الله عنهما، قَالَ: أمرنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بسبع، ونهانا عن سبع: أمَرَنَا بعيَادَة المَرِيض، وَاتِّبَاعِ الجَنَازَةِ، وتَشْمِيتِ العَاطسِ، وَإبْرار المُقْسِم، ونَصْرِ المَظْلُوم، وَإجَابَةِ الدَّاعِي، وَإِفْشَاءِ السَّلامِ، ونَهَانَا عَنْ خَواتِيمٍ أَوْ تَخَتُّمٍ بالذَّهَبِ، وَعَنْ شُرْبٍ بالفِضَّةِ، وَعَن الميَاثِرِ الحُمْرِ، وَعَن القَسِّيِّ، وَعَنْ لُبْسِ الحَريرِ والإسْتبْرَقِ وَالدِّيبَاجِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية: وَإنْشَادِ الضَّالَّةِ في السَّبْعِ الأُوَل.

Kutoka kwa Abuu ‘Umaarah Al-Baraa’ bin ’Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) ametuamuru kutekeleza mambo saba: Ametuamuru kuwazuru wagonjwa, kufuata jeneza, kumuombea aliyepiga chafya, kuamini kiapo, kumnusuru aliyedhulumiwa, kuitikia mwaliko na kutoa na kueneza salamu. Na ametukataza kuvaa pete ya dhahabu, kunywa kwenye chombo cha fedha, kupanda shogi la hariri nyekundu, Al-Qasiyy, kuvaa hariri, Istabraq na dibaji.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine: “Na kusaidia kupata kilichopotea mambo saba yaliyotajwa mwanzo.”

 

 

Share