08-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miongoni Mwa Hayaa Zake Alistahi Maswahaabiyaat Katika Kuwaelekeza Jinsi Ya Kutwaharisha Hedhi

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

00-Miongoni Mwa Hayaa Zake Alistahi Maswahaabiyaat

Katika Kuwaelekeza Jinsi Ya Kutwaharisha Hedhi

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alimstahi mwanamke aliyemjia kumuuliza swala la hedhi yake, basi kwa kusitahi, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifunika uso wake baada ya kumjibu mwanamke huyo. Hadiyth inaelezea:

 

 عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ سَأَلَتِ امْرَأَةٌ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَيْفَ تَغْتَسِلُ مِنْ حَيْضَتِهَا قَالَ فَذَكَرَتْ أَنَّهُ عَلَّمَهَا كَيْفَ تَغْتَسِلُ ثُمَّ تَأْخُذُ فِرْصَةً مِنْ مِسْكٍ فَتَطَهَّرُ بِهَا ‏.‏ قَالَتْ كَيْفَ أَتَطَهَّرُ بِهَا قَالَ: ((تَطَهَّرِي بِهَا ‏.‏ سُبْحَانَ اللَّهِ)) ‏.‏ وَاسْتَتَرَ - وَأَشَارَ لَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ بِيَدِهِ عَلَى وَجْهِهِ  قَالَ: قَالَتْ عَائِشَةُ وَاجْتَذَبْتُهَا إِلَىَّ وَعَرَفْتُ مَا أَرَادَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا أَثَرَ الدَّمِ ‏.‏ وَقَالَ ابْنُ أَبِي عُمَرَ فِي رِوَايَتِهِ فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا آثَارَ الدَّمِ ‏.‏

 Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mwanamke alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vipi kuoga kujitwaharisha baada ya kumaliza hedhi yake. Akataja kuwa alimfundisha vipi kuoga kisha akamwambia achukue kipande cha pamba aweke misk  kwa ajili ya kujitwaharisha. Aksema: Vipi nijitwaharishe nacho? Akasema: ((Jitwaharishe nacho Subhaana Allaah!)) (Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)   akajifunika uso wake. Sufyaan bin ‘Uyaynah akaonyesha jinsi alivyojifunika uso wake. Akasema ‘Aaishah: Nikamvuta mwanamke kwangu kwani nilifahamu alivyokusudia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikasema: Pakaza pamba hiyo katika sehemu zenye athari ya damu. Na Ibn ‘Umar katika Hadiyth yake (ametaja maneno ya ‘Aaishah)  Pakaza katika sehemu zenye athari ya damu.  [Muslim]

 

 

 

Share