040-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Msafiri Akipukusa Kisha Akawasili Mjini Kwake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Twahara

 

040-Msafiri Akipukusa Kisha Akawasili Mjini Kwake

 

Alhidaaya.com

 

 

Ikiwa msafiri atapukusa juu ya khufu zake siku moja na usiku wake au zaidi kisha akawasili kwake, ni lazima azivue khufu zake, aoshe miguu yake anapotawadha, kisha atakuwa na hali ile ile ya mkazi.

 

Na ikiwa msafiri amepukusa kwa muda wa chini ya siku na usiku wake, basi inajuzu kwake anapowasili mjini akamilishe muda uliosalia wa siku moja na usiku wake, kisha ni lazima azivue. 

 

Ibn Al-Mundhir amenukulu Ijma’a ya kila Mwanachuoni anayezungumzia kwa kuainisha kuhusu muda wa kupukusa. [Al-Awsatw (1/446)].

 

 

Share