03-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nguzo Za Kiislamu Ni Tano
Hadiyth Ya 3
بني الإسلام على خمس
Nguzo Za Kiislamu Ni Tano
عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Abdir-Rahmaan Abdillaah Ibn 'Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zaka na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]