10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa Harufu Nzuri Mno Ya Manukato

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

10-Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa  Harufu Nzuri Mno Ya Manukato  

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عن أَنَسٌ رضي الله عنه قال: مَا شَمِمْتُ عَنْبَرًا قَطُّ وَلاَ مِسْكًا وَلاَ شَيْئًا أَطْيَبَ مِنْ رِيحِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلاَ مَسِسْتُ شَيْئًا قَطُّ دِيبَاجًا وَلاَ حَرِيرًا أَلْيَنَ مَسًّا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Sijapatapo kusikia ‘ambar au misk wala harufu yoyote nyengine yenye harufu nzuri kama harufu ya mwili wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na sijapatapo kugusa makhmeli wala hariri iliyo laini kabisa kulikono mwili wa Rasuli wa Allaah  Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)) [Muslim]

 

 

‘Ambar = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri kabisa.

 

Misk = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri.  Miski ziko rangi mbili:  nyeupe na nyeusi. Hii ndio iliyotajwa katika Sunnah kwa ajili ya wanawake kujitwaharisha hedhi zao.

 

 

 Na pia:

 

 عن جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلاَةَ الأُولَى ثُمَّ خَرَجَ إِلَى أَهْلِهِ وَخَرَجْتُ مَعَهُ فَاسْتَقْبَلَهُ وِلْدَانٌ فَجَعَلَ يَمْسَحُ خَدَّىْ أَحَدِهِمْ وَاحِدًا وَاحِدًا - قَالَ - وَأَمَّا أَنَا فَمَسَحَ خَدِّي - قَالَ - فَوَجَدْتُ لِيَدِهِ بَرْدًا أَوْ رِيحًا كَأَنَّمَا أَخْرَجَهَا مِنْ جُؤْنَةِ عَطَّارٍ ‏.‏

Kutoka kwa Jaabir Bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya mwanzo kisha akatoka kwenda kwa ahli zake nami nikatoka kwenda naye. Akakutana na watoto (njiani). Akawagusa mashavu yao mmmoja mmoja. Akanigusa mimi pia shavu langu nikahisi ubaridi au harufu ya mkono wake kama vile umetolewa kutoka mfuko wa mafuta ya manukato mazuri.”  [Muslim

Share