281-Aayah Na Mafunzo: Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah: 281 : Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾

281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa

 

 

Mafunzo:

 

 

Wengi kati ya ‘Ulamaa wamekiri kwamba hii ni Aayah ya mwisho  kuteremshwa. Na miongoni mwa Salaf waliokiri ni Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), na Sa’iyd  bin Jubayr (رحمه الله) kwa Riwayaah mbalimbali kwamba baada kuteremshwa Aayah hii yakapatika masiku kadhaa kisha akafariki Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

Na Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema: “Hii ni Aayah ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur-aan, na ikafanywa ni hatima ya hukmu hizi za maamrisho na makatazo kwa sababu humo mna ahadi za kutenda mema na kheri, na only la kutenda maovu, na kwamba anayejua kwamba yeye atarejeshwa kwa Allaah, basi Atamlipa kwa dogo na kubwa (aliyoyatenda) na yaliyodhahiri na ya siri na kwamba Allaah Hatomdhulumu uzito wa chembe ya hardali (au atomu), basi itamwajibika awe na raghbah (utashi, matumaini) na khofu. Na bila kuyajua hayo moyoni kutakuwa hakuna sababu ya kuyatekeleza.”

 

Share