051-Hiswnul-Muslim: Du’aa Anayoomba Mgonjwa Aliyekata Tamaa Ya Kupona

Hiswnul-Muslim

051-Du’aa Anayoomba Mgonjwa Aliyekata Tamaa Ya Kupona

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[150]

أللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي وَارْحَمْـني وَأَلْحِقْـني بِالرَّفـيقِ الأّعْلـى

 

Allaahummagh-fir-liy war-hamniy wa alhiqniy birrafiyqil a’-laa

 

Ee Allaah, Nighufurie na Unirehemu na Unikutanishe na waja walio katika daraja za juu[1]

 

 

 

[151]

 

 

جَعَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ يُدْخِلُ يَدَيْهِ فِي الْماءِ، فَيَمْسَحُ بِهِما وَجْهُهُ وَيُقُولُ:

 

لاَ إِلَهَ إِلاَّ الله، إِنَّ لِلْمَـوْتِ لَسَكَـراتٍ

 

Wakati Nabiy (صلى الله عليه وسلم) anakufa alikuwa akiingiza mikono yake ndani ya maji kisha akipangusa kwayo uso wake na akisema:

 

لاَ إِلَهَ إِلاَّ الله، إِنَّ لِلْمَـوْتِ لَسَكَـراتٍ

Laa ilaaha illa-Allaah, inna lilmawti sakaaraat

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah, hakika kifo bila shaka kina uchungu[2]

 

 

 

 [152]

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَاللّهُ أَكْبَـر، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَريكَ لهُ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ لهُ المُلكُ ولهُ الحَمْد، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَلا حَـوْلَ وَلا قُـوَّةَ إِلاّ بِالله.

 

Laa ilaaha illa-Allaahu wa Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu, laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, laa ilaaha illa-Allahu Lahul-Mulku walahul-Hamdu, laa ilaaha illa-Allaahu walaa hawla walaa quwwata illaa biLLaahi

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah Mpweke Hana mshirika, hapana mwabudiwa iwa wa haki ni Allaah, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake, hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah[3]

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya ’Aaisha (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy (7/10) [4440], Muslim (4/1893) [2444],  At-Tirmdihiy na  Ahmad.

[2]Hadiyth ya ’Aaisha (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (8/144) [4440] na Hadiyth ya siwaak

[3]Abu Sa’iyd Al-Khudriyy na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

 مَنْ قَالَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ فَقَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَأَنَا أَكْبَرُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي لا شَرِيكَ لِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا لِيَ الْمُلْكُ وَلِيَ الْحَمْدُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ ، قَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِي ؛ وَكَانَ يَقُولُ : مَنْ قَالَهَا فِي مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ

((Atakayesema:Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa”, Rabb wake amemsadiki, Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Nami ni Mkubwa”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Peke Yangu”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Mpweke Hana mshirika”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi Peke Yangu Sina mshirika”. Na akisema; “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Ufalme ni Wangu na Himdi ni Zangu”. Na Akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa Zangu”. Alikuwa (Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akisema: Atakayesema hayo akiwa mgonjwa akafariki, moto hautamla)) -At-Tirmidhiy [3430], Ibn Maajah [3794], na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله). Taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/152), Swahiyh Ibn Maajah (2/317), Swahiyh At-Targhiyb (3481)

 

Share