Al-Lajnah Ad-Daaimah: Aashuraa: Kuchinja Siku Ya ‘Aashuraa Imo Katika Shariy'ah?

 

Kuchinja Siku Ya ‘Aashuraa Imo Katika Shariy'ah?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kuchinja mnyama siku fulani au wakati maalumu kila mwaka kwa vile kuna watu wengine huamini kuwa kuchinja tarehe 27 Rajab au 6 Swafar au 15 Shawwaal na  10 Muharram kuwa inawakurubisha kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  na kwamba ni tendo la ‘ibaadah.  Je, matendo haya ni sahihi? Na je, ni katika Sunnah au bid’ah inayokwenda kinyume na mafunzo sahihi ya kiislamu na mwenye kufanya hatolipwa thawabu kwa tendo hili?

 

 

JIBU:

 

‘Ibaadah zote zinazomkurubisha mtu kwa Allaah ni tawqifiyy (kutokana na  mafunzo ya Quraan na Sunnah na sio kutokana na rai za watu). 

 

Hakuna nukuu kutoka Quraan wala Hadiyth sahihi inayotaja uchinjaji wa mnyama katika masiku yaliyotajwa ya miezi hiyo, wala Maswahaba (Radhwiya-Allaahu ‘anhum) hawakufanya hayo na kwa hiyo kufanya hivyo ni bid’’ah. 

 

Imenukuliwa katika Hadiyth Swahiyh kwamba

 

( مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ 

 “Atakayezusha katika jambo letu hili (la Dini) lolote ambalo halimo humo litarudishwa.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

Share