31-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

31-Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao. [An-Nisaa: 80]

 

Na katika Hadiyth:

عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ‏"‏‏.‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

 Na katika Hadiyth nyengine:

 

عن عبدالله بن عمر رضي الله عنه أنه كان يومًا من الأيامِ عندَ رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلمَ وهو في نفرٍ من أصحابِه فقال: ((ألستم تعلمون أنِّي رسولُ اللهِ؟)) قالوا: "بلى يا رسولَ اللهِ نشهدُ أنك رسولُ اللهِ" قال: ((ألستم تعلمونَ أن اللهَ تعالَى أنزلَ في كتابِه أنَّ مَن أطاعَني فقد أطاع اللهَ؟)) قالوا: "بلى نشهدُ أن مَن أطاعَك فقد أطاع اللهَ" قال: ((فإنَّ مِن طاعتي أن تطيعوا أئمَّتَكم فإن صلُّوا قُعودًا فصلُّوا قُعودًا))

‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba siku moja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi alipokuwa na baadhi ya Maswahaba akasema: ((Je si mnajua kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah?)) Wakasema: “Bila shaka ee Rasuli wa Allaah tunashuhudia kuwa wewe ni Rasuli wa Allaah.”  Akasema: ((Je, si mnajua kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ameteremsha katika Kitabu Chake kuwa “Atakayenitii mimi atakuwa amemtiia Allaah?” Wakasema: “Bila shaka tunashuhudia kuwa atakayekutii wewe atakuwa amemtii Allaah.” Akasema: ((Miongoni mwa kunitii ni Imaam wenu wanaposwali wakiwa wamekaa kitako, basi nanyi mswali kwa kukaa kitako)) [Musnad Ahmad ni Hadiyth Swahiyh taz Asw-Swahiyh Al-Musnad, (761), na riwaayah nyengine Taz Swahiyh Ibn Hibbaan (2109), Swiffatusw-Swalaah ya Al-Albaaniy (1/87)]

 

 

 

Share