Wali Wa Sosi Ya Tuna

Wali Wa Sosi Ya Tuna

VIPIMO                                                    

Sosi Ya tuna

Tuna (samaki/jodari) -  2 Vikopo

Vitunguu (kata kata)  - 4

Nyanya zilizosagwa -  5

Nyanya kopo -  3 Vijiko vya supu

Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes)  -  4

Dengu (chick peas) -  1 kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa   1 Kijiko cha  supu

Hiliki -  1/4 kijiko cha chai

Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu

Chumvi    -  kiasi

Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai

Mraba ya supu ya kuku au nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).

 

Wali:
Mchele  -    3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Mdalasini -  2 Vijiti

Karafuu -  chembe 5

Zaafarani - kiasi

*Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) -  1/2 Kikombe

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 1. Kosha Mchele na roweka.
 2. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando.
 3. Kaanga viazi, epua
 4. Punguza mafuta, kaanga nyanya.
 5. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi.
 6. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi.
 7. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali.
 8. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.
 9. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika  chombo cha kupikia katika jiko (oven)
 10. Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali.
 11. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu).
 12. Funika wali na upike katika jiko moto wa 450º kwa muda wa kupikika wali. Epua upakue.

 * Jirsh ni komamanga kavu. Zioshwe vizuri kutoa vumbi au tumia zabibu kavu (raisins)

 

 

 

 

Share