Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

 

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja

Vitunguu maji - 3

Karoti - 2

Siagi - 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili
 2. Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
 3. Kwaruza karoti (grate) weka kando.
 4. Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
 5. Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
 6. Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
 7. Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo. 
 8. Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

 

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu

Ndimu - 1

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kukaangia - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
 2. Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
 3. Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
 4. Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali. 

 

Share