Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Du’aa Na Du’aa Hutakabaliwa

 

Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Du’aa Na Du’aa Hutakabaliwa

 

Alhidaaya.com

 

 

Du’aa ni ‘ibaadah kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

 

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))

Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa]: 

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni))

 

Amesema: ((Du’aa ndio ‘ibaadah)) kisha akasoma: 

 

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾

Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike.  [Ghaafir: 60] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Juu ya hivyo, du’aa ni ‘amali tukufu kabisa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنْ الدُّعَاءِ))  

Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((Hakuna kitu kitukufu mbele ya Allaah kama du’aa))  [Swahiyh Adab Al-Mufrad]

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiadhimisha ‘amali ya kuomba du’aa khasa katika mwezi wa Ramadhwaan kwa sababu zifuatazo:

 

 

1-Aayah ya amrisho la kumuomba du’aa Allaah (سبحانه وتعالى) imo baina ya Aayaat za Swiyaam Mwezi wa Ramadhwaan. Imeanza Aayah namba 183 mpaka Aayah namba 185 kisha ikaja kauli Yake (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

 

Kisha ikaendelea kuhusu Swiyaam:

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ  ….

Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu…. [Al-Baqara: 187]

 

 

2-Du’aa ya mwenye Swawm hairudishwi bali inatakabaliwa:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ، الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ، وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ يَرْفَعُهَا اللَّهُ دُونَ الْغَمَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَتُفْتَحُ لَهَا أَبْوَابُ السَّمَاء،وَيَقُولُ بِعِزَّتِي لأَنْصُرَنَّكِ وَلَوْ بَعْدَ حِينٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam (kiongozi) muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa, Anainyanyua Allaah bila ya mawingu Siku ya Qiyaamah na inafunguliwa milango ya mbingu na Anasema: “Kwa Utukufu Wangu, Nitakunusuru japo baada ya muda.)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (2526) Ibn Maajah, Ahmad]

 

Pia katika Hadiyth:

 

عّنْ أَنسْ بِنْ ماَلِكْ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): ((ثَلاَثُ دَعْواتِ لاَ تُرَدُّ: دَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ، وَدَعْوَةُ الصَّائِم،  وَدَعْوَةُ الْمُسَافَرَ))

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ((Du’aa za watatu hazirudishwi; du’aa ya mzazi kwa mwanawe, na du’aa ya mwenye Swawm, na du’aa ya msafiri)) [Al-Bayhaqiy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3032) na katika Asw-Swahiyhah (1797)]

 

 

3-Muislamu anapaswa aombe du’aa kwa wingi katika Ramadhwaan kujikinga na Moto wa Jahannam na kuomba Jannah (Pepo), kwa sababu milango ya Moto inafungwa na milango ya Jannah inafunguliwa na mashaytwaan wanafungwa minyororo:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا دَخَلَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ جَهَنَّمَ وَسُلْسِلَتْ الشَّيَاطِينُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Inapoingia Ramadhwaan, milango ya Jannah hufunguliwa, milango ya Moto wa Jahannam hufungwa na mashaytwaan hufungwa minyororo)) [Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy]

 

 

Pia mwenye Swawm Ramadhwaan ameahidiwa kughufuriwa madhambi yake pindi akifunga kwa iymaan na akataraji malipo:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ رواه البخاري ، ومسلم (.

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayefunga Ramadhwaan kwa Iymaan na  kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

4-Kuomba du’aa kila usiku wa Ramadhwaan kujaaliwa kuwa miongoni mwa watakaoepushwa na Moto kwa sababu kila inapofika usiku, kuna waja ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajaalia kuwa ni wenye kuepushwa na Moto:

 

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( إِنَّ لِلَّهِ عِنْدَ كُلِّ فِطْرٍ عُتَقَاءَ ، وَذَلِكَ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ ) . رواه أحمد (21698) وابن ماجه ( 1643 ) . وصححه الشيخ الألباني في " صحيح ابن ماجه " .

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika katika baada ya kufuturu (Magharibi kuendelea), Allaah Ana watu wa kuwaepusha na Moto, na hivyo ni katika kila usiku.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (1340)]

 

Na pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( إِذَا كَانَ أَوَّلُ لَيْلَةٍ مِنْ شَهْرِ رَمَضَانَ صُفِّدَتْ الشَّيَاطِينُ ، وَمَرَدَةُ الْجِنِّ ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ ، فَلَمْ يُفْتَحْ مِنْهَا بَابٌ ، وَفُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ ، فَلَمْ يُغْلَقْ مِنْهَا بَابٌ ، وَيُنَادِي مُنَادٍ : يَا بَاغِيَ الْخَيْرِ أَقْبِلْ ، وَيَا بَاغِيَ الشَّرِّ أَقْصِرْ ، وَلِلَّهِ عُتَقَاءُ مِنْ النَّارِ ، وَذَلكَ كُلُّ لَيْلَةٍ ) . رواه الترمذي ( 682 ) وابن ماجه ( 1642 ) . وحسَّنه الشيخ الألباني في " صحيح الجامع

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Inapofika usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhwaan mashaytwaan hufungwa, na majini huzuiliwa, na milango ya  Moto hufungwa, haufunguliwi mlango hata mmoja humo, na Milango ya Jannah hufunguliwa,  na hakuna hata mmoja unaofungwa, kisha mwenye kunadi hunadi: “Ee mtafutaji kheri, kurubia! Ee mtafuta maovu, acha! Na Allaah Anao ambao wa kuwaacha huru kutokana na Moto na hivyo ni kila usiku. [Ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (682), Swahiyh Ibn Maajah (1339), Swahiyh Al-Jaami’ (759)]

 

 

5- Kwa vile Muislamu hana budi kutawadha kwa ajili ya Swalaah zake, basi pindi akimaliza kutawadha aombe du’aa ambayo milango ya Jannah (Pepo) inakuwa wazi: 

 

 

 عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ الْوُضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إلاَّ فُتِحَتْ لَهُ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ))

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab  (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayetawadha akatia vizuri wudhuu wake, kisha akasema:

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ،

“Ash-hadu anlaa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu [Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake] ila atafunguliwa milango minane ya Jannah ataingia wowote apendao)) [Ibn Maajah – Swahiyh Ibn Maajah (385)]

 

 

6-Kwa vile katika Ramadhwaan Muislamu anahimizwa kuamka usiku kwa ajili ya Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kuswali), basi anapoamka ana fadhila za kuomba du’aa:

 

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي، أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ، فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit  (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: 

 

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، رَبِّ اغْفِرْ لِي

 

Laa ilaaha illa-Allaah  Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLlaah,   Rabbigh-fir-liy

 

(Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah, ee Allaah, nighufurie) au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)) [Al-Bukhaariy na wengineo] 

 

Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Huteremka kila siku thuluthi ya mwisho ya usiku kuwaitikia waja Wake du’aa zao:

 

عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْه)ُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ:  ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآَخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Rabb wetu Tabaaraka wa Ta’aalaa) Huteremka [kwa namna inavyolingana na utukufu Wake] kila siku katika mbingu ya dunia [ya kwanza] inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ananitaka jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Vile vile kuna Du’aa katika Saa ya usiku ambayo hairudi bali inataqabaliwa:

 

عَنْ جَابِرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ)  قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ: ((إِنَّ فِي اللَّيْلِ لَسَاعَةً لاَ يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ خَيْرًا مِنْ أَمْرِ الدُّنْيَا وَالآَخِرَةِ إِلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: ((Hakika katika usiku bila shaka kuna saa haimuwafikii mtu Muislamu anayemwomba Allaah khayr katika mambo ya dunia au Aakhirah ila Atampa, na hiyo ni kila usiku)) [Muslim (757), Swahiyh Al-Jaami’ (2130)]

 

 

7- Du’aa Wakati Wa Kusoma Qur-aan kwani Ramadhwaan ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan:

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ  

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili).  [Al-Baqarah: 184]

 

Na pia Muislamu anaposoma Qur-aan, anapopitia Aayah zenye kubashiriwa Jannah, basi aiombe Jannah, na anapopitia Aayah za Moto, aombe kujikinga nao. Na anapopitia Aayah zenye maonyo ya adhabu za Allaah aombe kujikinga na adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى)  duniani na Aakhirah na aombe Rahmah za Allaah. Hivyo ni kufuata mafunzo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):   

 

عن ‏حُذَيْفَةَ بِنْ اليمان (رضي الله عنه): أنَّ النَّبِيَّ‏ ‏(صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) كَانَ ‏إِذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ سَألَ، وَإِذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍاسْتَجَارَ، وَإِذَا مَـرَّ بِآيَةٍ فِيهَـا تنزيهٌ للَّهِ سبَّحَ

Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa anapopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya adhabu aliomba kujikinga, na alipopitia Aayah zenye kumtakasa Allaah alimsabbih)) [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]

 

Pia,

كان إذا مرَّ بآيةِ خوفٍ تعوَّذَ، و إذا مرَّ بآيةِ رَحمةٍ سألَ، و إذا مرَّ بآيةٍ فيها تَنزيهُ اللهِ سبَّحَ

Alikuwa anapopitia Aayah ya khofu, alijikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya kumtakasa Allaah, alimsabbih)) [Swahiyh Al-Jaami’ (4782)]

 

Pia:

 

‏أَنَّهُ ‏صَلَّى إِلَى جَنْبِ النَّبِيِّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) ‏لَيْلَةً فَقَرَأ فَكَانَ إذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍ وَقَفَ وَتَعَوَّذَ وَإذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ وَقَفَفَدَعَا

Kwamba ameswali pembeni na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  usiku mmoja, akasoma akawa kila anapopitia Aayah ya adhabu alisita na akajikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah alisita akaomba. [Swahiyh An-Nasaaiy (1007)]

 

 

 

8-Usiku unaojulikana kwa Laylatul-Qadr, ni usiku mtukufu mno ambao humo majaaliwa ya mja yanaandikwa na pia du’aa inataqabaliwa:

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Atakayesimama usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy (1910) na Muslim (760)]  

 

Na du’aa makhsusi ya Laylatul-Qadr ni kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّهَا قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ وَافَقْتُ لَيْلَةَ الْقَدْرِ مَا أَدْعُو؟ قَالَ: ((تَقُولِينَ: اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها)  amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, nitakapojaaliwa kupata Laylatul-Qadr niombe nini?   Akasema: “Sema:

اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي

 

Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'afwa fa'-fu 'anniy. [Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe))  [Swahiyh Ibn Maajah (3119)]

 

Bonyeza viungo vifuatavyo uendelee kupata faida tele:

 

Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

Sayyidul Istighfaar Du’aa Bora Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Na Fadhila Za Kuomba Tawbah

 

Basi hakika Ramadhwaan ni fursa adhimu kwa Muislamu kuomba du’aa apate kutakabaliwa haja zake. Usikose kamwe kila siku kijiombea du’aa za kheri kwa ajili ya Aakhirah na dunia yako, na kuwaombea, wazazi, ndugu na jamaa na Waislamu kwa ujumla.

 

 

Share