Nyama Ya Mbuzi Ya Kukaanga Kwa Bizari Mchanganyiko

AttachmentSize
Image icon nyama_ya_mbuzi_10286.jpg73.43 KB

Nyama Ya Mbuzi Ya Kukaanga Kwa Bizari Mchanganyiko

 

 

 

Vipimo 

 

Nyama mbuzi -  kilo 1  

Tangawizi na thomu ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Jira (bizari ya pilau) – kijiko 1 cha chai

Dania (gilgilani) – kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi 

Bizari mchanganyiko – vijiko 2 vya chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai  

Ndimu – 2 kamua

Mafuta – vijiko 3 ya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Katika bakuli, changanya nyama pamoja na chumvi, tangawizi, thomu, jira, dania, weka katika moto uchanganye vizuri.
  2. Tia maji kiasi tu ya kutoshea kuivisha nyama bila kubakia supu.
  3. Tia katika bakuli, bizari mchanganyiko, pilipili manga, ndimu, changanya vizuri, kisha iwache ikolee viungo kwa muda kiasi nusu saa au zaidi.
  4. Weka mafuta katika kikaangio kisichogandisha, mimina nyama, kaanga mpaka igeuke rangi ya brown ya kuchomeka nyama.
  5. Epua chuja mafuta, tayari kuliwa na saladi upendayo.

 

  Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

Share