055-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila na Ubora wa Kuupa Nyongo Ulimwengu wa Kukinai Kwa Kichache na Ubora wa Ufakiri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر

055-Mlango Wa Fadhila na Ubora wa Kuupa Nyongo Ulimwengu wa Kukinai Kwa Kichache na Ubora wa Ufakiri

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢٤﴾

Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake (kuivuna); tahamaki amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (ishara, hoja) kwa watu wanaotafakari. [Yuwnus: 24]

 

 

وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾ الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

Na wapigie mfano wa uhai wa dunia kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika kwayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha yakawa makavu yaliyovurugika yanapeperushwa na upepo. Na Allaah daima ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa kwa kila kitu. Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini. [Al-Kahf: 45-46]

 

اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾

Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka.  Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri. [Al-Hadiyd: 29]

 

 

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾

Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri. [Aal-'Imraan: 14]

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۖ وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٥﴾

Enyi watu!  Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah. [Faatwir: 5]

 

أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾ حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾ ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾ كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾

Kumekughafilisheni kutafuta wingi. Mpaka muingie makaburini. Laa hasha! Mtakuja kujua. Kisha laa hasha! Mtakuja kujua. Laa hasha! Lau mngelijua ujuzi wa yakini. [At-Takaathur: 1-5]

 

 

وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾

Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua! [Al-'Ankabuwt: 64]

 

 

 

والآيات في الباب كثيرة مشهورة . وأما الأحاديث فأكثر مِنْ أن تحصر فننبِّهُ بطرف منها عَلَى مَا سواه .

Na ayah katika mlango huu ni nyingi na mashuhuri. Ama Hadiyth ni nyingi zaidi hata hazihesabiki na hapa tuataja baadhi yake.

 

 

 

 

Hadiyth – 1

عن عمرو بن عوف الأنصاري رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم بَعَثَ أَبَا عبيدة بنَ الجَرَّاح رضي الله عنه إِلَى الْبَحْرَيْنِ يَأتِي بِجِزْيَتِهَا ، فَقَدِمَ بمَالٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ ، فَسَمِعَتِ الأَنْصَارُ بقُدُومِ أَبي عُبيْدَةَ ، فَوَافَوْا صَلاَةَ الفَجْرِ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا صَلَّى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، انْصَرفَ ، فَتَعَرَّضُوا لَهُ ، فَتَبَسَّمَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِيْنَ رَآهُمْ ، ثُمَّ قَالَ: (( أظُنُّكُمْ سَمعتُمْ أنَّ أَبَا عُبَيْدَةَ قَدِمَ بِشَيْءٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ ؟ )) فقالوا : أجل ، يَا رسول الله، فقال : (( أبْشِرُوا وَأَمِّلْوا مَا يَسُرُّكُمْ، فَوالله مَا الفَقْرَ أخْشَى عَلَيْكُمْ ، وَلكِنِّي أخْشَى أنْ تُبْسَط الدُّنْيَا عَلَيْكُمْ كَمَا بُسِطَتْ عَلَى مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ ، فَتَنَافَسُوهَا كَمَا تَنَافَسُوهَا ، فَتُهْلِكَكُمْ كَمَا أهْلَكَتْهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Al 'Awfy Al Answaary (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimpeleka Abu 'Ubaydah 'Amir bin al-Jarraah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Bahrayn kukusanya Jizyah yao. Akarudi na mali kutoka Bahrayn. Ma-Ansaar walipata habari ya kurudi kwa Abu 'Ubaydah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) hivyo wakaswali Swalaah ya Alfajiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomaliza kuswali Rasuli wa Allaah, walikuja kwake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitabasamu alipowaona, kisha akasema: "Nadhania mumesikia ya kwamba Abu 'Ubaydah amerudi na kitu kutoka Bahrayn?" Wakasema: "Ndio, ee Rasuli wa Allaah!" Akasema: "Furahini, na tarajieni vitu vitakavyo wafurahisha. Wa-Allaahi! Siwaogopeeni ufukara, lakini naogopa kukunjuliwa dunia juu yenu, kama walivyo kunjuliwa waliokuwa kabla yenu, mkaishindania kama walivyoishindania, ikakuangamizeni nyinyi kama ilivyowangamiza wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : جلس رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى    الْمِنْبَرِ ، وَجَلَسْنَا حَوْلَهُ ، فقال : (( إنَّ ممَّا أخَافُ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِي مَا يُفْتَحُ عَلَيْكُمْ مِنْ زَهْرَةِ الدُّنْيَا وَزِينَتِهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Alikaa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye mimbar nasi tukakaa duara (tukiwa tumemzunguka), akasema: "Kwa hakika yale ninayowaogopea nyinyi baada yangu ni kufunguliwa kwenu utajiri na kuvutiwa na dunia na mapambo yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( إنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرَةٌ وَإنَّ الله تَعَالَى مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا، فَيَنْظُرُ كَيْفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاءَ )) رواه مسلم.

Impokewa kutoka kwa Abu Saiyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika dunia ni tamu na kijani (imejaa utajiri) na Allaah Ta'aalaa atawafanya nyinyi kuwa makhalifa humo na atawaangalia kwa yale mnayofanya. Hivyo tahadharini na dunia na wanawake." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Hakuna starehe isipokuwa starehe ya Aakherah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أنس رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَتْبَعُ الْمَيِّتَ ثَلاَثَةٌ : أهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَمَلُهُ : فَيَرْجِعُ اثْنَانِ ، وَيَبْقَى وَاحِدٌ : يَرْجِعُ أهْلُهُ وَمَالُهُ وَيبْقَى عَمَلُهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hufuata maiti mambo matatu: Watu wake, mali yake na amali yake. Viwili hurudi na kubakia jambo moja tu: Hurudi watu wake na mali yake na kubakia amali yake." [Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يُؤْتَى بِأنْعَمِ أهْلِ الدُّنْيَا مِنْ أهْلِ النَّارِ يَوْمَ القِيَامَةِ ، فَيُصْبَغُ في النَّارِ صَبْغَةً، ثُمَّ يُقَالُ : يَا ابْنَ آدَمَ ، هَلْ رَأيْتَ خَيْراً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ نَعِيمٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لاَ وَاللهِ يَا رَبِّ ، وَيُؤْتَى بِأشَدِّ النَّاسِ بُؤسَاً في الدُّنْيَا مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ ، فَيُصْبَغُ صَبْغَةً في الجَنَّةِ ، فَيُقَالُ لَهُ : يَا ابْنَ آدَمَ ، هَلْ رَأيْتَ بُؤساً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ شِدَّةٌ قَطُّ ؟ فيَقُولُ : لاَ وَاللهِ ، مَا مَرَّ بِي بُؤْسٌ قَطُّ ، وَلاَ رَأيْتُ شِدَّةً قَطُّ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Anas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ataletwa mtu mwenye neema zaidi katika watu duniani Siku ya Qiyaamah na kuchovya Motoni mara moja. Kisha kutasemwa: 'Ee binadamu! Je, umeona kheri yeyote? Je, ulipata neema yeyote?' Atasema: 'La! Wa-Allaahi! Sijapata, ee Rabb wangu.' Ataletwa maskini zaidi duniani katika watu wa Peponi, Atatiwa mara moja Peponi, Kutasemwa: 'Ee binadamu! Je, ulipata shida yeyeote?, Atasema: 'Wa-Allaahi! Sijapata tabu, sikupata shida yeyeote." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن المُسْتَوْرِد بن شَدَّاد رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا الدُّنْيَا في الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ أُصْبُعَهُ في اليَمِّ، فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ ! )) رواه مسلم.

Imepokewa kutoka kwa Al-Mustawrid bin Shaddaad (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dunia si chochote katika Aakherah isipokuwa ni kama mfano wa mtu anayetia kidole chake katika bahari. Naangalie kiasi gani cha maji kinachukua." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ بالسُّوقِ وَالنَّاسُ كَنَفَتَيْهِ ، فَمَرَّ بِجَدْيٍ أَسَكَّ مَيِّتٍ ، فَتَنَاوَلَهُ فَأَخَذَ بِأُذُنِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( أَيُّكُم يُحِبُّ أنْ يَكُونَ هَذَا لَهُ بِدرْهَم ؟ )) فقالوا : مَا نُحِبُّ أنَّهُ لَنَا بِشَيْءٍ وَمَا نَصْنَعُ بِهِ ؟ ثُمَّ قَالَ : (( أَتُحِبُّونَ أَنَّهُ لَكُمْ ؟ )) قَالُوا : وَاللهِ لَوْ كَانَ حَيّاً كَانَ عَيْباً ، إنَّهُ أسَكُّ فَكَيْفَ وَهُوَ ميِّتٌ ! فقال : (( فوَاللهِ للدُّنْيَا أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ هَذَا عَلَيْكُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita sokoni pamoja na Swahaaba zake alimuona mbuzi mdogo amekufa na masikio yake yamekatwa. Alikishika katika masikio na kuuliza: "Nani anayemtaka (huyu mbuzi aliyekufa) kwa dirhamu moja?" Wakasema: "Hatutaki huyo awe ni wetu kwa chochote (hata bure). Na je, tutamfanya nini? " Kisha akasema: "Je, mngependa awe wenu bure?" Wakasema: "Wa-Allaahi! Hata kama angekuwa hai angekuwa na kasoro, vipi akiwa maiti?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Wa-Allaahu! dunia ni duni zaidi mbele ya Allaah kuliko juu yenu." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي ذر رضي الله عنه ، قَالَ : كُنْتُ أَمْشِي مَعَ النَّبي صلى الله عليه وسلم في حَرَّةٍ   بِالمَدِينَةِ ، فَاسْتَقْبَلَنَا أُحُدٌ ، فقال : (( يَا أَبَا ذَرٍّ )) قلت : لَبَّيْكَ يَا رسولَ الله . فقال : (( مَا يَسُرُّنِي أنَّ عِنْدِي مِثْلَ أُحُدٍ هَذَا ذَهَباً تَمْضي عَلَيَّ ثَلاَثَةُ أيّامٍ وَعِنْدِي مِنْهُ  دِينَارٌ ، إِلاَّ شَيْءٌ أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ ، إِلاَّ أنْ أقُولَ بِهِ في عِبَادِ الله هكذا وَهَكَذَا وَهكَذَا )) عن يَمِينِهِ وعن شِمَالِهِ وَمِنْ خَلْفِهِ ، ثُمَّ سَارَ ، فقال : (( إنَّ الأَكْثَرينَ هُمُ الأَقَلُّونَ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلاَّ مَنْ قَالَ بالمَالِ هكَذَا وَهكَذَا وَهكَذَا )) عن يمينِهِ وعن شِمَالِهِ وِمنْ خَلْفِهِ (( وَقَلِيلٌ مَاهُمُ )) . ثُمَّ قَالَ لي : (( مَكَانَكَ لاَ تَبْرَحْ حَتَّى آتِيكَ )) ثُمَّ انْطَلَقَ في سَوادِ اللَّيْلِ حَتَّى تَوَارَى ، فَسَمِعْتُ صَوتاً ، قَدِ ارْتَفَع ، فَتَخَوَّفْتُ أنْ يَكُونَ أحَدٌ عَرَضَ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَأرَدْتُ أنْ آتِيهِ فَذَكَرتُ قَوْله : (( لا تَبْرَحْ حَتَّى آتِيَكَ )) فلم أبْرَحْ حَتَّى أتَاني ، فَقُلْتُ : لَقَدْ سَمِعْتُ صَوتاً تَخَوَّفْتُ مِنْهُ ، فَذَكَرْتُ لَهُ ، فقال :   (( وَهَلْ سَمِعْتَهُ ؟ )) قلت : نَعَمْ ، قَالَ : (( ذَاكَ جِبريلُ أتَانِي . فقال : مَنْ مَاتَ مِنْ أُمَّتِكَ لاَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّةَ )) ، قلت : وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : (( وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa natembea na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika majabali Madiynah tukatokea Uhud. Akaniita: "Ee Abu Dharr." Nikasema: "Labbayka ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Lau ningekuwa na dhahabu mfano wa Uhud hii, Ipite kwangu suku tatu nibaki nayo hata dinari moja, isipokuwa kuiweka kwa ajili ya deni. Ila Ningeigawa kwa waja wa Allaah hivi na hivi na hivi', kulia, kushoto na nyuma." Kisha akatembea akasema: "Hakika wenye vingi duniani ndio wenye kidogo zaidi Siku ya Qiyaamah, isipokuwa wanaotumia mali hivi na hivi na hivi', kulia na kushoto na nyuma, "Nao wao ni wachache." Baada ya hapo akaniambia: "Hapo hapo usiondoke hadi nikujie." Kisha alitembea katika giza nene hadi akapotea. Nilisikia sauti kubwa, nikahofia mtu kumtokea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), isiwe amepatikana na jambo baya. Nilitaka kumuendea nikakumbuka kauli yake: "Usiondoke hadi nikujie." Sikuondoka mpaka aliporudi, nikasema: "Nilisikia sauti kubwa sana nikaihofia, nikamkumbusha." Akasema: "Uliisikia?" Nikasema: "Ndio." Akasema: "Huyu alikuwa ni Jibriyl alinijia, akaniambia: 'Atakayekufa katika Ummah wako hamshirikishi Allaah na chochote ataingia Peponi." Nikauliza: "Hata akizini na kuiba?" Akasema: "Hata kama atazini na ataiba." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه  ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْ كَانَ لِي مِثْلُ أُحُدٍ ذَهَباً ، لَسَرَّنِي أنْ لاَ تَمُرَّ عَلَيَّ ثَلاَثُ لَيالٍ وَعِنْدِي مِنْهُ شَيْءٌ إِلاَّ شَيْءٌ أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau ningekuwa na dhahabu mfano wa Mlima Uhud, ingenifurahisha kutopita siku tatu nami nimebakia na chochote isipokuwa kitu nakiweka kwa ajili ya kulipa madeni." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أسْفَلَ مِنْكُمْ وَلاَ تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ ؛ فَهُوَ أجْدَرُ أنْ لاَ تَزْدَرُوا نِعْمَةَ الله عَلَيْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم .

وفي رواية البخاري : (( إِذَا نَظَرَ أَحَدُكُمْ إِلَى مَنْ فُضِّلَ عَلَيْهِ في المَالِ وَالخَلْقِ ، فَلْيَنْظُرْ إِلَى مَنْ هُوَ أسْفَل مِنْهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwangalie wa chini yako, wala usiangalie wa juu yako, hilo ni hakika hutopuuza neema za Allaah juu yako." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Anapoangalia mmoja wenu aliyefadhilishwa juu yake kwa mali na sura nzuri, basi amtizame aliye chini yake."

 

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( تَعِسَ عَبْدُ الدِّينَارِ ، وَالدِّرْهَمِ ، وَالقَطِيفَةِ ، وَالخَمِيصَةِ ، إنْ أُعْطِيَ رَضِيَ ، وَإنْ لَمْ يُعْطَ لَمْ يَرْضَ )) رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ameangamia mwenye kutafuta dinari na dirhamu na nguo zenye manyoa na mavazi ya thamani. Wanapopatiwa huridhia na wasipopatiwa basi hawaridhiki." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ سَبعِينَ مِنْ أهْلِ الصُّفَّةِ ، مَا منهُمْ رَجُلٌ عَلَيْهِ رِدَاءٌ : إمَّا إزارٌ ، وَإمَّا كِسَاءٌ ، قَدْ رَبَطُوا في أعنَاقِهِمْ ، فَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ نِصْفَ السَّاقَيْن ، وَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ الكَعْبَيْنِ ، فَيَجْمَعُهُ بِيَدِهِ كَراهِيَةَ أنْ تُرَى عَوْرَتُهُ . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Hakika nimeona Swahaaba sabiini katika watu wa Swuffah hakuna hata mmoja miongoni mwao mwenye kikoi: Ima ni shuka wamezifunga katika shingo zao, katika hizo kuna zinazofika katikati ya miguu, katika hizo kuna zinazofika kongo mbili, kwa hiyo wakazikusanya kiunoni kwa kuchukia kuonekana uchi wao." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 14

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ ، وَجَنَّةُ الكَافِرِ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Dunia ni jela ya Muumini na Pepo ya kafiri." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : أخذ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبَيَّ ، فقال : (( كُنْ في الدُّنْيَا كَأنَّكَ غَرِيبٌ ، أَو عَابِرُ سَبيلٍ )) .

وَكَانَ ابن عُمَرَ رضي الله عنهما ، يقول : إِذَا أمْسَيتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ الصَّبَاحَ ، وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ المَسَاءَ ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ ، وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) akisema kwamba: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishika mabega yangu akisema: 'Kuwa duniani kama kwamba wewe ni mgeni au mpita njia.' Na Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) alikuwa akisema: 'Na ufikiwapo na usiku usitaraji kuwa uatafika hadi asubuhi, na ukipambazukiwa usitaraji kuwa utafika hadi jioni. Na faidika na (wakati wa) siha yako kabla ya (wakati wa) uhai wako kabla ya kufa kwako." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 16

وعن أَبي العباس سهل بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فقال : يَا رسولَ الله ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أحَبَّنِي اللهُ وَأحَبَّنِي  النَّاسُ ، فقال : (( ازْهَدْ في الدُّنْيَا يُحِبّك اللهُ ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبّك   النَّاسُ )) حديث حسن رواه ابن ماجه وغيره بأسانيد حسنة .

Imepokewa kutoka kwa Abui 'Abbaas Sahl bin Sa'd As-Sa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe mimi amali ambayo nikiifanya Allaah atanipenda na watu watanipenda." Akasema: "Upe nyongo ulimwengu atakupenda Allaah, na vipe nyongo viliomo mikononi mwa watu watakupenda watu." Hadiyth Hasan [Ibn Maajah na wengineo kwa isnad nzuri]

 

 

Hadiyth – 17

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : ذَكَرَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه ، مَا أَصَابَ النَّاسُ مِنَ الدُّنْيَا ، فَقَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَظَلُّ الْيَوْمَ يَلْتَوِي مَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: Alitaja 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) yale yaliyowafikia watu katika hii dunia, akasema: "Hakika nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akipitisha siku zake akiwa na njaa hana hata tende mbaya ya kuondoa njaa yake." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 18

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوفي رسول الله صلى الله عليه وسلم، وَمَا في بَيْتِي مِنْ شَيْءٍ يَأكُلُهُ ذُو كَبِدٍ إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ في رَفٍّ لي ، فَأكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ  عَلَيَّ ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) amesema: "Aliaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na hakukuwa katika nyumba chakula cha sawa (kwa watu kula) isipokuwa mtama kidogo katika stoo yangu ambao nilikuwa nikiutumia kwa muda. Baadae nilitaka kuupima lakini ukawa umemalizika." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 19

وعن عمرو بن الحارث أخي جُوَيْرِيّة بنتِ الحارِث أُمِّ المُؤْمِنِينَ ، رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا تَرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِيناراً ، وَلاَ دِرْهَماً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ أَمَةً ، وَلاَ شَيْئاً إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيضَاءَ الَّتي كَانَ يَرْكَبُهَا ، وَسِلاَحَهُ ، وَأرْضاً جَعَلَهَا لاِبْنِ السَّبِيلِ صَدَقَةً . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Amri bin Al-Haarith, kakake Juwayriyyah bint Al-Haarith, Mama wa Waumini ambaye amesema: "Hakuacha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kufariki hata dinari moja wala dirhamu wala mjakazi wala kijakazi wala kitu kingine chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akipanda na silaha zake na ardhi aliyoiacha kama swadaqah kwa wasafiri." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 20

وعن خَبابِ بن الأَرَتِّ رضي الله عنه، قَالَ : هَاجَرْنَا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَلْتَمِسُ وَجْهَ اللهِ تَعَالَى ، فَوَقَعَ أجْرُنَا عَلَى اللهِ ، فَمِنَّا مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَأكُل منْ أجْرِهِ شَيْئاً ، مِنْهُمْ : مُصْعَبُ بن عُمَيْرٍ رضي الله عنه ، قُتِلَ يَوْمَ أُحُد ، وَتَرَكَ نَمِرَةً ، فَكُنَّا إِذَا غَطَّيْنَا بِهَا    رَأْسَهُ ، بَدَتْ رِجْلاَهُ ، وَإِذَا غَطَّيْنَا بِهَا رِجْلَيْهِ ، بَدَا رَأسُهُ ، فَأمَرَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم ، أنْ نُغَطِّي رَأسَهُ ، وَنَجْعَل عَلَى رِجْلَيْهِ شَيْئاً مِنَ الإذْخِرِ ، وَمِنَّا مَنْ أيْنَعَتْ لَهُ ثَمَرَتُهُ ، فَهُوَ يَهْدِبُهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Khabbaab bin Al-Aratt (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa amesema: "Tulihama pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya radhi za Allaah Ta'aalaa, ujira wetu ukatoka kwa Allaah, Miongoni mwetu kuna waliokufa kabla ya kula ujira wao, Miongoni mwao ni Mus'ab bin 'Umayr (Radhwiyah Allaah 'anhu) ameuwawa siku ya Uhud, ameacha shuka tukimfunika nayo uso wake miguu yake inakuwa wazi, na tulipomfunika miguu, uso wake umakuwa wazi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tumfunike uso wake na kumfunika miguu yake na Idhkhir (aina ya mmea ambao ni maarufu na wenye harufu nzuri). Na miongoni mwetu kuna waliopata neema kwa wingi (hapa duniani) nao wakafurahia hilo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 21

وعن سهلِ بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَوْ كَانَت الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ الله جَنَاحَ بَعُوضَةٍ ، مَا سَقَى كَافِراً مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama uliwengu ungekuwa na thamani sawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, hangempatia kafiri maji ya kunywa hata kiasi cha mkono mmoja." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 22

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( أَلاَ إنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا ، إِلاَّ ذِكْرَ اللهِ تَعَالَى ، وَمَا وَالاهُ ، وَعالِماً وَمُتَعَلِّماً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Jueni ya kuwa hii dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyo ndani yake ispokuwa kumtaja Allaah Ta'aalaa na vile Anavyovipenda na wanavyuoni na wanafunzi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hasan]

 

 

Hadiyth – 23

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا في الدُّنْيَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwe ni wenye kupapia raslimali (zisizohamishika) na hivyo kupendelea dunia." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hasan]

 

 

Hadiyth – 24

وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : مَرَّ عَلَيْنَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَنَحْنُ نعالِجُ خُصّاً لَنَا ، فَقَالَ : (( مَا هَذَا ؟ )) فَقُلْنَا : قَدْ وَهَى ، فَنَحَنُ نُصْلِحُهُ ، فَقَالَ : (( مَا أرَى الأَمْرَ إِلاَّ أعْجَلَ مِنْ ذَلِكَ )) . رواه أَبو داود والترمذي بإسناد البخاري ومسلم ، وقال الترمذي : (( حديثٌ حسنٌ صحيحٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita tukiwa tunatengeneza paa (la nyumba ya mbao), akasema: "Munafanya nini?" Tukasema: "Paa limekuwa dhaifu nasi tunalitengeneza." Akasema: " Ninaona amri hiyo (Siku ya Qiyaamah) inafika kwa haraka zaidi kuliko jambo lenu hili." [Abu Dawuud na At-Tirmidhiy kwa Isnaad ya Al-Bukhaariy na Muslim, na akasema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hassan Swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 25

وعن كعب بن عياض رضي الله عنه  ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( إنَّ لِكُلِّ أُمَّةٍ فِتْنَةً ، وفِتْنَةُ أُمَّتِي : المَالُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ صحيحٌ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Ka'b bin 'Iyaadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika kila Ummah una fitnah (mtihani) na fitnah ya Ummah wangu ni mali." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 26

وعن أَبي عمرو ، ويقالُ : أَبو عبدِ الله ، ويقالُ : أَبو ليلى عثمان بن عفان رضي الله عنه  : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ في سِوَى هذِهِ الخِصَالِ : بَيْتٌ يَسْكُنُهُ ، وَثَوْبٌ يُوارِي عَوْرَتَهُ ، وَجِلْفُ الخُبز وَالماء )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Amri (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Inasemwa ni Abu 'Abdillaah, na inasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanadamu hana haki ya kuwa na zaidi ya vitu aina tatu: nyumba atakayoishi, na mavazi ya kusitiri uchi wake na kipande cha mkate na maji." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 27

وعن عبدِ الله بن الشِّخِّيرِ - بكسر الشينِ والخاء المعجمتين - رضي الله عنه، أنه قَالَ : أتَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ يَقْرَأُ : ( أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ) قَالَ : (( يَقُولُ ابْنُ آدَمَ : مَالِي ، مالي ، وَهَلْ لَكَ يَا ابْنَ آدَمَ مِنْ مَالِكَ إِلاَّ مَا أكَلْتَ فَأفْنَيْتَ ، أَو لَبِسْتَ فَأَبْلَيْتَ ، أَوْ تَصَدَّقْتَ فَأَمْضَيْتَ ؟! )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Ash-Shikhiyr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anasoma: "Al-Haakumut Takaathur." Akasema: "Mwanadamu anasema: Mali yangu, mali yangu. Kwani wewe mwanadamu una mali isipokuwa kile ulichokula kikapotea au ulichovaa kikamalizika au ukatoa swadaqah na ukatanguliza mbele yako?" [Muslim]

 

 

Hadiyth – 28

وعن عبدِ الله بن مُغَفَّل رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رجل للنبي صلى الله عليه وسلم :
يَا رسولَ الله ، وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ ، فَقَالَ : (( انْظُرْ مَاذَا تَقُولُ ؟ )) قَالَ : وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ ، ثَلاَثَ مَرَّات ، فَقَالَ : (( إنْ كُنْتَ تُحِبُّنِي فَأَعِدَّ لِلْفَقْرِ تِجْفَافاً ، فإنَّ الفَقْرَ أسْرَعُ إِلَى مَنْ يُحِبُّني مِنَ السَّيْلِ إِلَى مُنْتَهَاهُ ))
رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mughaffal (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Mtu alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi mimi nakupenda." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Angalia usemalo." Akasema: "Wa-Allaahi mimi nakupenda." Mara tatu. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ikiwa unanipenda jitayarishe kwa ufukara, kwani ufukara ni haraka zaidi kwa menye kunipenda, kuliko mafuriko na mwisho wake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 29

وعن كعب بن مالك رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  : (( مَا ذِئْبَانِ جَائِعَانِ أُرْسِلا في غَنَمٍ بِأفْسَدَ لَهَا مِنْ حِرْصِ المَرْءِ عَلَى المَالِ وَالشَّرَفِ لِدِينهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ka'abbin Maalik (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbwa mwitu wawili wenye njaa watakao pelekwa kwenye mkao (kundi) kwa kondoo hawatatia hasara zaidi kuliko pupa ya mtu kwa mali na utukufu kwa Dini yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 30

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : نَامَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  عَلَى حَصيرٍ ، فَقَامَ وَقَدْ أثَّرَ في جَنْبِهِ ، قُلْنَا : يَا رَسُولَ اللهِ ، لَوْ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً . فَقَالَ : (( مَا لِي وَلِلدُّنْيَا ؟ مَا أَنَا في الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa Rasuli wa sallam (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilala mara moja juu ya majani ya mtende na alipoamka alama za majani hayo yalikuwa yanaonekana kwenye mwili wake. Tukamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, tukutayarishie godoro laini kwa ajili yako?" Akasema: "Sina haja na mambo ya dunia. Mfano wangu hapa duniani ni kama mpandaji anapumzika chini ya kivuli cha mti, kisha akaanza tena safari na kuuacha mti." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh] 

 

 

Hadiyth – 31

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يدْخُلُ الفُقَرَاءُ الْجَنَّةَ قَبْلَ الأَغْنِيَاءِ بِخَمْسِمئَةِ عَامٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mafakiri wataingia Peponi miaka mia tano kabla ya matajiri." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 32

وعن ابن عباس وعِمْرَانَ بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ: (( اطَّلَعْتُ في الجَنَّةِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا الفُقَرَاءَ ، وَاطَّلَعْتُ في النَّارِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا النِّسَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ من رواية ابن عباس ، ورواه البخاري أيضاً من رواية عِمْرَان بن الحُصَيْن .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas na 'Imraan Ibn Al-Huswayn (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilichungulia Peponi nikaona watu wake wengi ni mafakiri. Na nikatizama Motoni nikaona watu wake wengi ni wanawake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

 

 

Hadiyth – 33

وعن أسامة بن زيد رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( قُمْتُ عَلَى بَابِ الجَنَّةِ ، فَكَانَ عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا المَسَاكِينُ ، وَأصْحَابُ الجَدِّ مَحبُوسُونَ ، غَيْرَ أنَّ أصْحَابِ النَّارِ قَدْ أُمِرَ بِهِم إِلَى النَّارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilisimama kwenye mlango wa Pepo, ikawa wengi wanaoingia ni masikini, na wenye utajiri wamezuiwa, isipokuwa watu wa Motoni wameamriwa kuingizwa motoni." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 34

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أصْدَقُ كَلِمَةٍ قَالَهَا شَاعِرٌ كَلِمَةُ لَبِيدٍ : ألاَ كُلُّ شَيْءٍ مَا خَلاَ اللهَ بَاطِلُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Neno la kweli alilosema mshairi ni neno la Labiyd: "Tanabahi kwamba kila kitu mbali na Allaah ni batili." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share