Sphaghetti Kwa Sosi Ya Kababu Za Nyama

Sphaghetti Kwa Sosi Ya Kababu Za Nyama

 

Vipimo vya Sosi

 

Vitungu vilivyokatwa - 2 Kiasi

Thomu iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu 

Nyanya ya kopo - 1 kopo

Nyanya ziliyosagwa - 3 Vikombe

Viungo vya Kiitali (Oregano,basil,thyme) - 1 Kijiko cha supu

Chumvi - Kiasi 

Pilipili manga ya unga - ½ Kijiko cha chai 

Figili mwitu (celery) na pilipili mboga - ½ Kikombe kila moja

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika sufuria kaanga vitungu kisha tia thomu.
  2. Tia Nyanya, nyanya kopo na viungo vyote.
  3. Tia pilipili mboga na figili mwitu na ukaange hadi zilainike.
  4. Tayarisha kababu za nyama ya kusaga katika supu.

 

Vipimo Vya Kababu

 

Nyama ya kusaga - 1 LB (Ratili)

Thomu na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu 

Chumvi - Kiasi

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 

Kotmiri iliyokatwa - Kiasi 

Garama Masala (bizari ya mchanganyiko) - 1 Kijiko cha chai 

Maji - 2 Gilasi

Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya vipimo vyote katika bakuli isipokuwa maji na kidonge  cha supu.
  2. Fanya viduara vidogo vya mchanganyiko wa nyama, weka kando.
  3. Chemsha maji kisha tia vidonge vya kababu vichemke.
  4. Tia kidonge cha supu (Stock)
  5. Zikishawiva mimina sosi uliyotayarisha juu ya hii supu ya kababu.
  6. Tayari kuliwa kwa kumwagiwa juu ya Spagetti.

Sphagetti

 

Chemsha Sphagetti kiasi ya 300 gm, zikiwiva chuja maji zikiwa tayari kuliwa na sosi pamoja na zaytuni ukipenda.

 

 

 

 

Share