Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Kwa Kamba Na Mboga Mchanganyiko
Chow Mein (Tambi Nene Za Kukaanga) Kwa Kamba Na Mboga Mchanganyiko
Vipimo
Noodles (Tambi nene za tayari) - 1 paketi
Mafuta ya ufuta (Sesame oil) - 3 vijiko vya supu
Kamba wakubwa (Prawns) - 2 LB
Nafaka mchanganyiko za barafu - 1 kikombe
Kabeji - ¼
sosi ya hardali (mustard) - 1 kijiko cha supu
Sosi ya soya (soy sauce) - 3 vijiko vya supu
Tomato ketchup - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) ilokunwa (grated) - 5 - 7 chembe
Tangawizi mbichi ilokunwa (grated) - 1 kipande
Paprika au pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai
Stock (kidonge cha supu) - 1
Maji ya moto - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
     
- Chambua noodles (tambi nene). Ikiwa ni zilozongoreka zikatekate kama kwenye picha.
 - Chemsha maji na zipike kama inavyoelezwa katika paketi. Au chemsha kiasi ya dakika chache tu zisiive sana hadi zikawa laini sana. Chuja maji. Changanya na siagi ili zisigandane.
 - Katakata kabeji vipande vya kiasi kwa urefu (grate) weka kando.
 - Weka karai katika moto. Tia mafuta.
 - Tia thomu na tangawizi mbichi ilokatwakatwa, kaanga kidogo kisha haraka tia sosi zote, tomato ketchup, paprika/pilipili nyekundu ya unga, chumvi endelea kukaanga kidogo.
 - Tia kamba (prawns waliosafishwa na kumenywa maganda) endelea kukaanga waive.
 - Tia nafaka mchanganyiko za barafu (frozen mixed peas) , changanya vizuri.
 - Weka kidonge cha supu (stock) katika kibakuli na tia maji ya moto ½ kikombe na uikoroge ivurugike iwe supu.
 - Mimina katika karai na changanya vizuri na mchanganyiko wa kamba. Acha muda wa dakika moja tu, kisha epua katika moto.
 - Kabla ya kupoa, tia kabejii na noodles/tambi na changanya vizuri pamoja vyote. Weka katika chombo cha kupakulia ikiwa tayari.
 
Kidokezo:
- Sio lazima kupatikana tambi za aina hiyo ya paketi. Muhimu ni tambi zozote nene (noodles)
 - Unaweza kutumia kitoweo kingine badala ya prawns.
 - Ikiwa hukupata nafaka za barafu, tumia za kawaida ila ziache ziive zaidi katika mchanganyiko.
 
    
    