070-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kutangamana na Watu, Kuhudhuria Mikusanyiko yao, Kushuhudia Kheri, Kushiriki Katika Vikao Vya Dhikri Pamoja nao, Kutembelea Wagonjwa, Kuhudhuria Jeneza Zao, Kukidhi Haja za Masikini Miongoni Mwao,

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل الاختلاط بالناس وحضور جُمَعِهم وجماعاتهم ،

ومشاهد الخير ، ومجالس الذكر معهم ، وعيادة مريضهم ، وحضور

جنائزهم ، ومواساة محتاجهم ، وإرشاد جاهلهم ، وغير ذلك من

مصالحهم لمن قدر عَلَى الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر ، وقمع

نفسه عن الإيذاء وصبر عَلَى الأذى

070-Mlango Wa Fadhila za Kutangamana na Watu, Kuhudhuria Mikusanyiko yao, Kushuhudia Kheri, Kushiriki Katika Vikao Vya Dhikri Pamoja nao, Kutembelea Wagonjwa, Kuhudhuria Jeneza Zao, Kukidhi Haja za Masikini Miongoni Mwao, Kuwaongoza Wajinga Wao na Mengineyo Katika Maslahi yao na Mwenye Kuweza au Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya na Kutoa Katika Nafsi Yake Uchafu na Kusubiri Maudhi na Shida.

 

 

Alhidaaya.com

 

 

اعْلم أنَّ الاختلاط بالنَّاسِ عَلَى الوجهِ الَّذِي ذَكَرْتُهُ هُوَ المختارُ الَّذِي كَانَ عَلَيْهِ رسول الله صلى الله عليه وسلم وسائر الأنبياء صلواتُ اللهِ وسلامه عَلَيْهِمْ ، وكذلك الخُلفاءُ الرَّاشدون ، ومن بعدَهُم مِنَ الصَّحَابَةِ وَالتَّابِعِينَ ، ومن بَعدَهُم من عُلَماءِ المُسلمين وأَخْيَارِهم ، وَهُوَ مَذْهَبُ أكثَرِ التَّابِعينَ وَمَنْ بَعدَهُمْ ، وبه قَالَ الشافعيُّ وأحمدُ وأكثَرُ الفقهاءِ رضي اللهُ عنهم أجمعين. قَالَ اللهُ تَعَالَى: ( وَتَعَاوَنُوا عَلَى البِرِّ وَالتَّقْوَى ) [ المائدة : 20 ] والآيات في معنى مَا ذكرته كثيرة معلومة .

Jua ya kwamba kutangamana na watu kwa njia niliyoitaja ndio yenye kupendeza. Ndio njia iliyokuwa ikifuatwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Manabii wote na hivyo hivyo Makhalifa waongofu na waliokuja baada yao miongoni mwa Swahaabah na Taabi'iyna. Na pia hiyo ilikuwa ndio sifa ya waliokuja baada yao miongoni mwa wanavyuoni Waislaamu na wabora wao. Na hii ndiyo madhehebu ya Taabi'iyna wengi na wala waliokuja baada yao. Na kwayo ndio amesema Ash-Shaafi'iy, na Ahmad na Mafakih wengi. Amesema Allaah Ta'aalaa: "Na shirikianeni katika wema na taqwa." [Al-Maaidah: 2]. Na kuna ayah nyingi katika mlango huu.

 

 

 

 

Share