071-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Unyenyekevu na Kuinamisha Bawa Waumini

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب التواضع وخفض الجناح للمؤمنين

071-Mlango Wa Unyenyekevu na Kuinamisha Bawa Waumini

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢١٥﴾

Na inamisha ubawa wako kwa anayekufuata miongoni mwa Waumini. [Ash-Shu'araa: 215]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ  ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri.[Al-Maaidah: 54]

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ ﴿١٣﴾

Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana namwanamme na mwanamke, na Tukakujaalieni  mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu. [Al-Hujuraat: 13]

 

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm: 32]

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾ أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾

Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari. Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah hatowafikishia kwa rahmah yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika. [Al-A'raaf: 48-49]

 

 

Hadiyth – 1

وعن عِيَاضِ بنِ حمارٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّ الله أوْحَى إِلَيَّ أنْ تَوَاضَعُوا حَتَّى لاَ يَفْخَرَ أحَدٌ عَلَى أحَدٍ ، وَلاَ يَبْغِي أحَدٌ عَلَى أحَدٍ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Iyaadh bin Himaar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah amenifunulia Wahyi kuwa nyenyekeeni hadi yoyote asijifakhiri mtu juu ya mwingine, wala yoyote asimfanye uadui mwingine." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : ((  مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ،وَمَا زادَ اللهُ عَبْداً بعَفْوٍ إِلاَّ عِزّاً، وَمَا تَوَاضَعَ أحَدٌ للهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللهُ (عزّ وجلّ )) رواه مسلم.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swadaqah haipunguzi mali; na Allaah anamuongezea utukufu mwenye kusamehe. Na hanyenyekei yoyote kwa ajili ya Allaah  ('Azza wa Jalla) isipokuwa Allaah humnyanyua." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّهُ مَرَّ عَلَى صبيَانٍ ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ ، وقال : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يفعله . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alipita mbele ya watoto na akawasalimia. Na hapo akasema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : إن كَانَتِ الأَمَةُ مِنْ إمَاءِ المَدينَةِ لَتَأْخُذُ بِيَدِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَتَنْطَلِقُ بِهِ حَيْثُ شَاءتْ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alisema: "Kijakazi miongoni mwa vijakazi wa Madiynah alikuwa anaweza kuushika mkono wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akawa anakwenda naye popote anapotaka ili amweleze shida yake." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن الأَسْوَدِ بن يَزيدَ ، قَالَ : سُئِلَتْ عائشةُ رضي الله عنها مَا كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ فِي بَيْتِهِ ؟ قالت : كَانَ يَكُون في مِهْنَةِ أهْلِهِ – يعني : خِدمَة أهلِه – فإذا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ ، خَرَجَ إِلَى الصَّلاَةِ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Al-Aswad bin Yaziyd ambaye amesema, 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) aliulizwa: "Je, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya nini nyumbani?" Alisema: :Alikuwa akiwahudumikia na kuwasaidia watu wake wa nyumbani, lakini wakatika wa Swalaah unapofika alikuwa akitoka kwenda kuswali." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي رِفَاعَةَ تَميم بن أُسَيْدٍ رضي الله عنه ، قَالَ : انْتَهَيْتُ إِلَى رَسولِ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يخطب ، فقلت : يَا رسول الله ، رَجُلٌ غَريبٌ جَاءَ يَسْألُ عن دِينهِ لا يَدْرِي مَا دِينُهُ ؟ فَأقْبَلَ عَليَّ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وتَرَكَ خُطْبَتَهُ حَتَّى انْتَهَى إلَيَّ ، فَأُتِيَ بِكُرْسيٍّ ، فَقَعَدَ عَلَيْهِ ، وَجَعَلَ يُعَلِّمُنِي مِمَّا عَلَّمَهُ اللهُ ، ثُمَّ أَتَى خُطْبَتَهُ فَأتَمَّ آخِرَهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Rifaa'ah Tamim bin Usayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Nilifika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anakhutubu, nami nikamuuliza: 'Ee Rasuli wa Allaah! Mtu mgeni amekuja kuuliza kuhusu Dini yake kwani yeye hajui chochote kuhusu Dini yake?' Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinikabili na akaja kwangu. Aliletewa kiti, akakikalia. Akawa ananifundisha aliyofundishwa na Allaah. Kisha alijia hutuba yake akaitimiza." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أكَلَ طَعَاماً ، لَعِقَ أصَابِعَهُ الثَّلاَثَ . قَالَ : وقال : ((  إِذَا سَقَطَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيُمِط عنها الأَذى ، وليَأكُلْها وَلاَ يَدَعْها لِلشَّيْطان )) وأمرَ أن تُسلَتَ القَصْعَةُ ، قَالَ : ((  فإنَّكُمْ لاَ تَدْرُونَ في أيِّ طَعَامِكُمُ البَرَكَة )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akilamba vidole vyake vitatu baada ya kumaliza kula. Amesema Anas kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tonge la mmoja wenu likianguka basi aondoe uchafu ulioingia na kisha alile na wala asimwachie shetani." Na pia ameamuru kufuta kabisa sahani (aliyolia mmoja wenu) na akasema: "Hakika nyinyi hamujui ni chakula chenu kipi kina baraka." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا بَعَثَ الله نَبِيّاً إِلاَّ رَعَى الغَنَمَ )) قَالَ أصْحَابُهُ : وَأنْتَ ؟ فَقَالَ : ((  نَعَمْ ، كُنْتُ أرْعَاهَا عَلَى قَرَارِيطَ لأَهْلِ مَكَّةَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah hakutuma Nabiy, ila Nabiy huyo alichunga mbuzi." Wakasema Swahaaba zake: "Hata wewe?" Akasema: "Ndio, nilikuwa nikichunga kwa watu wa Makkah na nikilipwa Qaraarit." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لَوْ دُعِيتُ إِلَى كُراعٍ أَوْ ذِرَاعٍ لأَجَبْتُ ، ولو أُهْدِيَ إِلَيَّ ذراعٌ أَوْ كُراعٌ لَقَبِلْتُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau ningealikwa kwa chakula cha muundi au bega ningeitikia na lau ningepatiwa zawadi ya muundi au bega ningekubali (ningepokea)." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَتْ ناقةُ رسول الله صلى الله عليه وسلم العضْبَاءُ لاَ تُسْبَقُ ، أَوْ لاَ تَكَادُ تُسْبَقُ ، فَجَاءَ أعْرَابيٌّ عَلَى قَعودٍ لَهُ ، فَسَبَقَهَا ، فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَى الْمُسْلِمِينَ حَتَّى عَرَفَهُ ، فَقَالَ : ((  حَقٌّ عَلَى اللهِ أنْ لاَ يَرْتَفِعَ شَيْءٌ مِنَ الدُّنْيَا إِلاَّ وَضَعَهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Ngamia wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiitwa 'Adhbaa', naye hakuwa akimruhusu ngamia yeyote amshinde. Wakati mmoja alikuja bedui aliyekuwa na ngamia mchanga aliyempita ngamia wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Jambo hilo lilikuwa gumu sana kwa Waislamu mpaka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatambua hilo. Akasema: "Ni haki kwa Allaah kukutojikweza chochote duniani ila atakishusha." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

 

Share