Imaam Ibn Rajab: Muumini Lazima Atubie Kila Siku Kukhofia Mauti Na Kufufuliwa Na Madhalimu

Muumini Lazima Atubie Kila Siku Kukhofia Mauti Na Kufufuliwa Na Madhalimu

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Alllaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

Amesema Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Alllaah):

“Haimpasi Muumini kupambaukiwa na kufika jioni yake isipokuwa kwa Twabah, kwani hajui ni wakati gani mauti yatamshtukiza ni asubuhi au jioni au roho yake itachukuliwa wakati wa utiifu wake au wakati wa kumuasi kwake Allaah.

Hivyo basi atakayepambazukiwa au kufika jioni bila ya kufanya Tawbah mtu huyu yupo kwenye hatari kwani huogopea kukutana na Rabb wake akiwa hajatubia na hivyo basi kufufuliwa pamoja na wadhalimu, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   Anasema:

  وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾

Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. [Al-Hujuraat: 11]

 

[Latwaaif Al-Ma’aarif 458].

 

 

 

 

Share