Imaam Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy: Majani Ya Sidri (Kunazi) Ni Tiba Dhidi Ya Uchawi

 

Majani Ya Sidri (Kunazi) Ni Tiba Dhidi Ya Uchawi 

 

Imaam Al-Haafidwh Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Amesema Al-Hafidhw bin Hajar (Rahimahu Allaah): (Mtu) Achukue majani saba ya Sidri (Kunazi) (yaliyo) mabichi kisha ayatwange kati ya mawe mawili,  kisha ayachanganye na maji na (kisha) ayasomee Ayatul-Kursiyy na Al-Qawaaqil:  (Suwrah Al-Jinn, Al-Kaafiruwn, Al-Ikhlaasw, Al-Falaq, An-Naas)  kisha avivie (apulizie)  mara tatu na kisha ayaoge, basi,  itamuondoshea yote yaliyomsibu. Na ni nzuri pia kwa yule aliyezuiwa (ashindwaye kumuingilia) Ahli yake kwa uchawi."  [Fat-hul Baariy (10/233)]

 

 

Al-Qawaaqil ni Suwrah zinazoanzia na  قُلْ  nazo ni:

 

Al-Jinn (72), Al-Kaafiruwn (109), Al-Ikhlaasw (112), Al-Falaq (113), An-Naas (114)

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu Ruqya ya Sihri:

 

10-Ruqya: Kutafuta Shifaa: Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula

 

 

 

                     

 

Share