Halwa/Halua Ya Karoti

Halwa/Halua Ya Karoti

Vipimo

Karoti iliyoparuzwa - 3 vikombe vya chai

Sukari - 2 vikombe vya chai

Maziwa - 2 vikombe vya chai

Lozi  au korosho - 1 kikombe cha chai                                

zilizokatwa ndogo ndogo

Hiliki - ½ kijiko cha chai

Samli - 4 vijiko vya chai vidogo

 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Kaanga lozi  kwa ile samli kidogo ziweke pembeni.
  2. Tia maziwa, hiliki na sukari kwenye sufuria chemsha ikisha chemka mimina Karoti.
  3. Chemsha mpaka ikauke maziwa tia lozi.
  4. Mimina kwenya trei.
  5. Ikisha kupoa kata vipande. Tayari kwa kuliwa.
Share