Skip to main content

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

Hadiyth Ya 20

Ukorofi Ni Khulqa Mbaya

Alhidaaya.com

وَعَنْ عَائِشَةَ ‏رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا‏ قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {اَلشُّؤْمُ: سُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukorofi ni khulqa (tabia) mbaya.”  [Imetolewa na Ahmad na katika isnaad yake kuna udhaifu]

Faida:

Shari anazopata Mwana -Aadam ni kutokana na khulqa (tabia) zake mbaya. Hadiyth hii inaonyesha kuwa khulqa nzuri au mbaya za mtu zinatokana na chaguo lake binafsi.