21-Hadiyth Husnul-Khuluq: Muumini Ni Kioo Kwa Muumini Mwenzake Kwa Husnul-Khuluq

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 21

Muumini Ni Kioo Kwa Muumini Mwenzake Kwa Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمُؤْمِنُ مِرْآةُ اَلْمُؤْمِنِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini ni kioo cha ndugu yake Muumini.” [Imetolewa na Abuu Daawud kwa isnaad Hasan]

  

Faida:

 

Mtu anajifunza kuonekana kwake iwe ni uzuri au ubaya pindi anapojiangalia katika kioo. Vivyo hivyo, Muislaam ndio kioo cha Muislaam mwenzake na anatakiwa ajifunze kutoka kwa mwenzake kwa khulqa (tabia) alizonazo ili apendeze kwa Allaah na kwa watu baada ya kuondokana na khulqa yake mbaya.

 

 

Share