22-Hadiyth Husnul-Khuluq: Allaah Anamchukua Mwenye Khulqa Mbaya Za Maneno Maovu

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 22

Allaah Anamchukua Mwenye Khulqa Mbaya Za Maneno Maovu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ‏ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{إِنَّ اَللَّهَ يُبْغِضُ اَلْفَاحِشَ اَلْبَذِيءَ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ

وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ ‏رَفَعَهُ‏: {لَيْسَ اَلْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ، وَلَا اَللَّعَّانُ، وَلَا اَلْفَاحِشَ، وَلَا اَلْبَذِيءَ} وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَرَجَّحَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Anamchukia muovu, mwenye maneno mabaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]

 

Pia amepokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd marfuw’: “Muumini si mtukanaji, wala si mlaanifu, wala mchafu, wala si mwenye maneno mabaya.” [Na amesema ni Hasan na akaisahihisha Al-Haakim. Ad-Daaraqutwniy ameitilia nguvu kuwa ni Marfuw’]

 

Faida:

 

Hadiyth hii inatuelekeza kuwa si katika khulqa (tabia) ya Muumini kuwaita nduguze majina mabaya au kuwalaani. Hata hivyo inaruhusiwa kumtukana na kumlaani yule aliyelaaniwa na Allaah na Rasuli wake. Au kutaja kwa ujumla laana ya Allaah kwa makafiri. Watu wenye kufanya mambo mabaya na machafu. Vinginevyo si halaal kumlaani mtu kwa kumtaja jina lake.

 

 

 

Share