03-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Allaah Akimtakia Mja Wake Kheri Humjaali Ufaqahi Wa Dini

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 03

 

Allaah Akimtakia Mja Wake Kheri Humjaali Ufaqahi Wa Dini

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وَعَنْ مُعَاوِيَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ يُرِدِ اَللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي اَلدِّينِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Akimtakia mja Wake kheri Humjaalia ufaqihi (‘ilmu ya kina) katika Dini.” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

Faida:

 

Elimu ya halaal na haraam katika Shariy’ah inaitwa Fiqh. Maelezo haya yanaonesha utukufu na ukubwa wa somo hili muhimu. Kilichoelezwa hapa ni elimu ya Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

 

 

Share