Skip to main content

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

Hadiyth Ya 08 

Balighisheni Japo Aayah Moja Tahadharini Kumzulia Uongo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

Alhidaaya.com

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو العَاص (رضي الله عنهما) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً،  وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) البخاري

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr Al-‘Aasw (رضي الله عنهما)   kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Balighisheni (fikisheni) kutoka kwangu japo Aayah moja. Na simulieni kuhusu habari za Wana wa Israaiyl wala hakuna dhambi [ubaya]. Na mwenye kunizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni)). [Al-Bukhaariy]