20-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Mwenye ‘Ilmu Asifiche ‘Ilmu Yake Ili Aepukane Na Lijamu La Moto
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 20
Mwenye ‘Ilmu Asifiche ‘Ilmu Yake Ili Aepukane Na Lijamu La Moto
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ سُئِلَ عَنْ عِلْمٍ فَكَتَمَهُ أَلْجَمَهُ اللَّهُ بِلِجَامٍ مِنْ نَارٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ " .
Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayeulizwa jambo la kuhusiana na ‘ilmu (ya Dini) lakini alifiche, atafungwa lijamu la moto Siku ya Qiyaamah.” [At-Tirmidhy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (120)].