14-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutaka Msaada wa Allaah na Ushauri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الاستِخارة والمشاورة

14-Mlango Wa Kutaka Msaada wa Allaah na Ushauri

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ  ﴿١٥٩﴾

Na washauri katika mambo. [Aal-'Imraan: 159]

 

وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ ﴿٣٨﴾

Na jambo lao hushauriana baina yao. [Ash-Shuwraa: 38]

 

 

Hadiyth – 1

وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الاسْتِخَارَةَ في الأمُورِ كُلِّهَا كَالسُّورَةِ مِنَ القُرْآنِ ، يَقُولُ : (( إِذَا هَمَّ أحَدُكُمْ بِالأمْرِ ، فَلْيَركعْ ركْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الفَرِيضَةِ ، ثُمَّ ليقل : اللَّهُمَّ إنِّي أسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ ، وَأسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ ، وأسْألُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيْمِ ، فَإنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أقْدِرُ ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أعْلَمُ ، وَأنْتَ عَلاَّمُ الْغُيُوبِ . اللَّهُمَّ إنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأمْرَ خَيْرٌ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أمْرِي )) أَوْ قَالَ : (( عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ ، فاقْدُرْهُ لي وَيَسِّرْهُ لِي ، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ . وَإنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي )) أَوْ قَالَ : (( عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ ؛ فَاصْرِفْهُ عَنِّي ، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ ، وَاقْدُرْ لِيَ الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ ، ثُمَّ أرْضِنِي بِهِ )) قَالَ : (( وَيُسَمِّيْ حَاجَتَهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifundisha Istikhaarah (kutaka shauri kwa Allaah) katika mambo yote kama alivyokuwa akitufundisha Suwrah katika Qur-aan, akisema: "Anapotaka kufanya jambo mmoja wenu na aswali rakaa mbili zisizo za faradhi kisha asema: 'Allaahumma inniy Astakhiyruka Bi'ilmika wa Astaqdiruka Biqudratika wa As'aluka min Fadhwlikal 'Adhiym. Fainnaka Taqdiru walaa Aqdiru wa Ta'alamu walaa A'lamu wa Anta 'Allaamul Ghuyuub. Allaahumma in Kunta Ta'lamu anna hadhaal amru khayrul liy fiy Diyniy wa Ma'aashiy wa 'Aqibati Amriy (au alisema 'Aaajili amriy wa Aajilihi) Faqdurhu liy wa Yassirli Thumma Baarik liy Fiyhi. Wa in Kunta Ta'lamu anna Hadhaal amra Sharrul liy fiy Diyniy wa Ma'aashiy wa 'Aaqibati Amriy (au alisema 'Aajili amriy wa Aajilihi) Faswrifuhu wa swrifni 'anhu waqadur liyal Khayyra haythu kaana Thumma Radhdhiniy Bihi' (yaani Ee Allaah! Nakuomba uongozi kutokana na Ilimu Yako. Na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako. Na nakuomba katika Fadhila Zako kubwa, kwani Wewe una uwezo nami sina uwezo, Nawe unajua lakini mimi sijui, Nawe ni Mjuzi wa ghayb. Ee Allaah! Kama jambo hili (hapa unataja jambo lenyewe), Unalilijua, ni kheri kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na marejeo yangu (au alisema katika Dunia yangu na Aakhera yangu). Basi niamuliye nilifanye na Nisahilishie kisha unibarikie kwa hilo. Na kama Unavyofahamu likiwa jambo hili (utalitaja tena jambo lenyewe) ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na marejeo yangu (au alisema katika Dunia yangu na Aakhera yangu), basi liepushe nami, na uniepushe nalo, na Uniamulie lenye kheri popote litakapokuwa kisha Uniridhishe nalo." Amesema: "Kisha hutaja haja yake." [Al-Bukhaariy].

 

 

 

Share