Imaam Ibn Baaz: Hedhi: Kupunguza Nywele Na Kukata Kucha Katika Hedhi Inajuzu?

 

Kupunguza Nywele Na Kukata Kucha Katika Hedhi Inajuzu?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Je inapasa kwa mwanamke kupunguza nywele na kucha zake wakati wa hedhi yake?

 

 

JIBU:

 

Hapana neno katika hilo katika kukata kucha zake na kunyofoa nywele zake za kwapani au kuondoa kwa kutumia dawa. Akiwa katika hedhi au katika nifaas au akiwa na janaba. Na  kwa mwanamme ni juu yake kuondosha nywele hizi na hata akiwa katika janaba kama vile kunyofoa nywele za kwapani, na kunyoa nywele kwenye kinena (mavuzi), kupunguza masharubu na kukata kucha, makusudio ya haya yote ni kwamba hayashurutishi tohara.

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Ala Ad-Darb (10845)]

 

 

 

 

Share