16-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharakisha Kumlipia Deni Maiti na Kuharakisha Kumuandaa Isipokuwa Mauti Yake Yathibitike
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تعجيل قضاء الدَّين عن الميت
والمبادرة إِلَى تجهيزه إلا أن يموت فجأة فيترك حَتَّى يُتَيَقَّنَ مَوْتُه
16-Mlango Wa Kuharakisha Kumlipia Deni Maiti na Kuharakisha Kumuandaa Isipokuwa Mauti Yake Yathibitike
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( نَفْسُ المُؤْمِنِ مُعَلَّقَةٌ بِدَيْنِهِ حَتَّى يُقْضى عَنْهُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nafsi ya Muumini hutundikwa kwa deni lake mpaka lilipwe." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 2
وعن حُصَيْنِ بن وَحْوَحٍ رضي الله عنه : أنَّ طَلْحَةَ بْنَ البَرَاءِ بن عَازِبٍ رضي الله عنهما مَرِضَ ، فَأتَاهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَعُودُهُ ، فَقَالَ : (( إنِّي لاَ أرى طَلْحَةَ إِلاَّ قَدْ حَدَثَ فِيهِ المَوْتُ ، فآذِنُوني بِهِ وَعَجِّلُوا بِهِ ، فَإنَّهُ لاَ يَنْبَغِي لجِيفَةِ مُسْلِمٍ أنْ تُحْبَسَ بَيْنَ ظَهْرَانِيْ أهْلِهِ )) رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa Huswayn Wahwah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Twalhah bin Al-Baraa' alishikwa na ugonjwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja kumzuru na kusema: "Hakika mimi nadhania kuwa Twalhah yu karibu na umauti, hivyo anapofariki nifahamisheni na fanyeni haraka kumzika, kwani haifai kwa maiti ya Muislaamu kubaki kwa familia yake bila sababu yeyote." [Abuu Daawuwd]
