09-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila Ya Swalaah Ya Asubuhi Na Alasiri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل صلاة الصبح والعصر

09-Mlango Wa Fadhila Ya Swalaah Ya Asubuhi Na Alasiri

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي موسى رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ صَلَّى البَرْدَيْنِ دَخَلَ الجَنَّةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayeswali (katika nyakati za) baridi mbili (Alfajiri na Alasiri) ataingia Peponi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي زهير عُمارة بن رُؤَيْبَةَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ: سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لَنْ يَلِجَ النَّارَ أحَدٌ صَلَّى قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا )) يعني : الفَجْرَ والعَصْرَ . رواه مسلم .

Abuu Zuhayr 'Ummaarah bin Ruwaybah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hataingia Motoni yeyote anayeswali kabla ya kuchomoza kwa jua na kabla kuchwa jua (yaani Alfajiri na Alasiri)." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن جُنْدُبِ بن سفيان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ صَلَّى الصُّبْحَ فَهُوَ في ذِمَّةِ اللهِ ، فَانْظُرْ يَا ابْنَ آدَمَ ، لاَ يَطْلُبَنَّكَ اللهُ مِنْ ذِمَّتِهِ   بِشَيءٍ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuswali Swalaah ya Asubuhi yupo katika himaya ya Allaah (katika usalama na chini ya dhamana yake). Hivyo ee Bin Aadam usivunje dhamana ya Allaah kwa chochote." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَتَعَاقَبُونَ فِيكُمْ مَلاَئِكَةٌ بِاللَّيْلِ ، وَمَلاَئِكَةٌ بِالنَّهَارِ ، وَيجْتَمِعُونَ في صَلاَةِ الصُّبْحِ وَصَلاَةِ العَصْرِ ، ثُمَّ يَعْرُجُ الَّذِينَ بَاتُوا فِيكُمْ ، فَيَسْأَلُهُمُ اللهُ - وَهُوَ أعْلَمُ بِهِمْ - كَيْفَ تَرَكْتُمْ عِبَادي ؟ فَيقُولُونَ : تَرَكْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ ، وَأتَيْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kwake Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wanapishana kati yenu Malaaikah wakati wa usiku na Malaaikah wakati wa mchana na wanajikusanya pamoja katika Swalaah ya Alfajiri na Swalaah ya Alasiri. Kisha wale Malaaikah waliokuwa usiku pamoja nanyi wanapanda juu na Allaah anawauliza: 'Mumewaachaje waja wangu?' Nao watajibu: 'Tumewaacha wakiwa wanaswali, na tumekwenda kwao tena na tumewakuta wanaswali.' " [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن جرير بن عبد الله البَجَليِّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كُنَّا عِنْدَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم فَنَظَرَ إِلَى القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ ، فَقَالَ : (( إنَّكُمْ سَتَرَونَ رَبَّكُمْ كَمَا تَرَوْنَ هَذَا القَمَرَ ، لاَ تُضَامُونَ في رُؤْيَتهِ ، فَإنِ اسْتَطَعْتُمْ أنْ لاَ تُغْلَبُوا عَلَى صَلاَةٍ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ، فَافْعَلُوا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية : (( فَنَظَرَ إِلَى القَمَرِ لَيْلَةَ أرْبَعَ عَشْرَةَ )) .

Na Jariyr bin 'Abdillaah Al-Bajaliy (Radhwiya Allaah 'anhu) amesema: Tulikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku, akauangalia mwezi uliokamilika mduara wake, akasema: "Hakika mtamuona Rabb wenu kama mnavyouona mwezi huu wala hamtasumbuliwa (au kudhulimiwa) katika kumuona na kama mtaweza kuwa mnaswali (daima) Swalaah ya kabla ya kuchomoza jua na Swalaah ya kabla ya kuzama jua fanyeni." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Na katika riwaayah nyingine: "Akauangalia mwezi usiku wa tarehe kumi na nne (14)."

 

Hadiyth – 6

وعن بُرَيْدَة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَرَكَ صَلاَةَ العَصْرِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuacha Swalaah ya Alasiri basi imeharibika amali yake." [Al-Bukhaariy]

 

Share