001-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Taarifu Ya Vyakula

 

 

 

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Taarifu Ya Vyakula

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

·        Taarifu Ya Vyakula

 

 

"الأَطْعِمَةُ" ni wingi wa "طَعَامُ", na katika lugha ni kila kile kinacholiwa, na pia kila kinachotumika kama chakula kutokana na ngano, shayiri na tende.  Kinaingia ndani ya taarifu hii kila kinachozalishwa na ardhi kati ya mimea ya mazao na matunda, na pia wanyama wote wanaoliwa, ni sawa wa nchi kavu au wa baharini.

 

Fuqahaa wanatumia tamko la chakula "الأَطْعِمَةُ" kwa kila kinacholiwa na kila kinachonywewa, ni sawa yakiwa maji au vilevi.

 

Na maudhui ya vyakula ni anuani inayogusia vilivyo halali kuliwa, vilivyo makruhu, na vilivyoharamishwa.

 

 

 

Share