002-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Asili Ya Vyakula Vyote Ni Halali Mpaka Iwepo Dalili Ya Kuharamisha

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

 

 

·        Asili Ya Vyakula Vyote Ni Halali Mpaka Iwepo Dalili Ya Kuharamisha

 

1-  Allaah Amesema:

 

"هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا"

 

“Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini”.  [Al-Baqarah: 29].

 

2-  Amesema tena:

 

"يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا"

 

“Enyi watu!  Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri.”  [Al-Baqarah: 168].

 

3-  Na Amesema pia:

 

"وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ •  قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ"

 

“Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu.  Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu  •  Sema:  Nani aliyeharamisha Mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea Waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki?  Sema:  Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah.  Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua”.  [Al-A’araaf:  31, 32].

 

 

 

 

Share