003-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Hakiharamishwi Chakula Chochote Ila Kile Tu Alichokiharamisha Allaah Katika Kitabu Chake Au Kupitia Ulimi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

003-Hakiharamishwi Chakula Chochote Ila Kile Tu Alichokiharamisha Allaah Katika Kitabu Chake Au Kupitia Ulimi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   

 

 

 

 

1-  Allaah Amesema:

 

"وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ" ﴿١١٩﴾

 

“Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.  Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya elimu.  Hakika Rabb wako Yeye Anajua Zaidi wenye kutaadi.”  [Al-An’aam: 119].

 

2-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ ﴿٥٩﴾ وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ"﴿٦٠﴾

 

59.  Sema:  Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo ni haramu na halali?  Sema:  Je, Allaah Amekupeni idhini au mnamtungia (uongo) Allaah?  •  60.  Na nini dhana ya wale wanaomtungia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah?  Hakika Allaah bila shaka Ana fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru”.  [Yuwnus: 59, 60].

 

3-  Na Akasema:

 

"وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ"﴿١١٦﴾

 

116.  Na wala msiseme kwa ndimi zenu zinazopambia uongo:  Hii halali na hii haramu ili mumtungie Allaah uongo.  Hakika wale wanaomtungia Allaah uongo hawafaulu”.  [An-Nahl: 116].

 

 

4-  Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"‏إِنَّ أَعْظَمَ الْمُسْلِمِينَ فِي الْمُسْلِمِينَ جُرْمًا مَنْ سَأَلَ عَنْ شَىْءٍ لَمْ يُحَرَّمْ عَلَى الْمُسْلِمِينَ فَحُرِّمَ عَلَيْهِمْ مِنْ أَجْلِ مَسْأَلَتِهِ‏"

“Hakika Muislamu anayewafanyia Waislamu kosa kubwa zaidi, ni yule mwenye kuuliza kitu ambacho hakikuharamishwa kwa Waislamu, halafu wakaharamishiwa kwa sababu ya kuuliza kwake”. [Hadiyth Swahiyh.  [Imekharijiwa na Muslim (2358)].

 

5-  Na toka kwa Abu Hurayrah kwamba Nabiy (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"‏ذَرُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ فَإِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِسُؤَالِهِمْ وَاخْتِلاَفِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ فَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ فَخُذُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَىْءٍ فَانْتَهُوا"

 

“Niacheni kama nilivyokuacheni (msiniulize viswali visivyo na umuhimu), kwani hakika waliangamia waliopita kabla yenu kwa sababu ya maswali yao mengi na kwenda kwao kinyume dhidi ya Manabii wao.  Hivyo, nikiwaamuruni jambo, basi lifanyeni kiasi cha uwezo wenu, na nikiwakatazeni jambo, basi liacheni”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337)].

 

6-  Toka kwa Abud Dardaai ikiwa Marfuw’u:

 

"مَا أَحَلَّ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ فَهُوَ حَلاَلٌ ، وَمَا حَرَّمَ فَهُوَ حَرَامٌ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَافِيَةُ ، فإنً اللهَ لَمْ يَكُنْ نَسِيًّا ، ثُمً تَلاَ هذِهِ الآيَةِ: وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا"

 

“Alilohalalisha Allaah katika Kitabu Chake, basi hilo ni halali, na Aliloharamisha basi hilo ni haramu, na Alilolinyamazia, basi hilo ni msamaha Amekuachilieni, kwani Allaah haiwezekani Akawa Mwenye Kusahau.  Kisha Akasoma Aayah hii:  “Na Rabb wako Si Mwenye Kusahau kamwe.  [Maryam: 64].  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Al-Haakim (2/406) na Ad-Daaraqutwniy (2/137).  Ina Hadiyth wenza.  Angalia Jaami’ul ‘Uluwmi wal Hikam (1/276)].

 

 

 

 

 

Share