015-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli

 

Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa

 

 

 

05- Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa

 

Ni kama panya, nge, kunguru, mwewe, mbwa anayeng’ata watu ovyo, mjusi wa viambaza na nyoka.

 

1-  Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"خَمْسٌ فَوَاسِقُ يُقْتَلْنَ فِي الْحَرَمِ الْفَأْرَةُ وَالْعَقْرَبُ وَالْحُدَيَّا وَالْغُرَابُ وَالْكَلْبُ الْعَقُورُ "‏

 

“(Wanyama) watano wabaya huuliwa katika Al-Haram:  Panya, nge, mwewe (kengewa), kunguru na mbwa anayeuma watu ovyo”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (3314) na Muslim (1198)].

 

2-  Toka kwa Sa-‘ad bin Abiy Waqqaasw (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: 

 

"أَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ بِقَتْلِ الْوَزَغِ وَسَمَّاهُ فُوَيْسِقًا"

 

“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kumuua mjusi wa viambaza (mjusi kafiri), na akamwita  kuwa ni kijinyama kidogo hatari”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2238).  Ina Hadiyth mwenza kwa Al-Bukhaariy toka Hadiyth ya Ummu Shurayk].

 

3-  Toka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:

 

" كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ فِي غَارٍ وَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيْهِ :‏ ( وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفًا)‏ ‏.‏ فَنَحْنُ نَأْخُذُهَا مِنْ فِيهِ رَطْبَةً إِذْ خَرَجَتْ عَلَيْنَا حَيَّةٌ فَقَالَ : ‏"‏ اقْتُلُوهَا ‏"‏ ‏، فَابْتَدَرْنَاهَا لِنَقْتُلَهَا فَسَبَقَتْنَا ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ : ‏"‏وَقَاهَا اللَّهُ شَرَّكُمْ كَمَا وَقَاكُمْ شَرَّهَا‏"‏ ‏.‏

 

Tulikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika pango akiwa ameshateremshiwa (Wal Mursalaat ‘Urfan).  Na wakati tukiwa tunaisikiliza (suwrah) toka mdomoni mwake ikiwa bado mbichi mpya, mara ghafla akatutokezea nyoka mkubwa, na Rasuli hapo hapo akatuambia: “Muueni”.  Tukakimbizana haraka tuwahi kumuua lakini akawahi kutukimbia. Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam) akasema:  Allaah Amemlinda na shari yenu kama Alivyowalindeni nyinyi na shari yake”.

 

Na kwa vile pia viumbe hawa ni khabithi wanaowafanya watu wenye maumbile salama kuchefukwa na roho.

 

 

Share