016-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Mnyama Ambaye Allaah Au Rasuli Wamekataza Kumuua Si Halali Kuliwa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

 

Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli

 

016-Mnyama Ambaye Allaah Au Rasuli Wamekataza Kumuua Si Halali Kuliwa

 

 

 

 

 

06- Mnyama Ambaye Allaah Au Rasuli Wamekataza Kumuua Si Halali Kuliwa

 

Ni kama sisimizi, nyuki, hud-hud, tiva (shrikes) na chura.

 

1-  Toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema:

 

 "نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ قَتْلِ أَرْبَعِ مِنْ اَلدَّوَابِّ : اَلنَّمْلَةُ، وَالنَّحْلَةُ، وَالْهُدْهُدُ، وَالصُّرَدُ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuua viumbe wanne:  Sisimizi, nyuki, hud-hud na tiva (shirkes)”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na An-Nasaaiy (5/189), Ahmad (6/83) na wengineo].

 

 

2-  Toka kwa ‘Abdul Rahmaan bin ‘Uthmaan amesema:

 

"ذَكَرَ طَبِيبٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ دَوَاءً، وذَكَرَ الضِّفْدَعً يَجْعَلُ فِيْهِ، فَنَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ قَتْلِ الضِّفْدَع"

 

“Tabibu (daktari) alitaja mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) dawa, na akaeleza kwamba dawa hiyo anaitengeneza kutokana na chura.  Na hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakataza kuua chura”.  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Ahmad (15197), Ad-Daaramiy (1998) na Ibn Maajah (3223)]. 

 

Ash-Shawkaaniy amepinga amri ya kuua kitu au kukataza kukiua, iwe ndio katika sababu za kuharamisha kukila.  Akasema:  “Allaah Ambaye Ndiye Mwekaji sharia, Hakutueleza chochote kinachofidisha kuharamisha kukila kile ambacho Ameamuru kukiua, au kilichokatazwa kukiua mpaka iwe amri na katazo ni dalili juu ya hilo.  Hivyo hakuna kigezo chochote cha kulifanya hilo kuwa ni chimbuko kati ya machimbuko ya kuharamisha.  Bali ikiwa kilichoamriwa kuuawa au kilichokatazwa kuuawa ni katika vinavyoingia ndani ya duara la vichafu, basi uharamisho wake unakuwa kwa Aayah Tukufu.  Na kama si katika hivyo, basi kitakuwa ni halali kwa kutegemea msingi wa uasili wa uhalali kama ilivyogusiwa nyuma, na kuwepo dalili kuu juu ya hayo”.  [Naylul Awtwaar (8)].

 

 

Share