Skip to main content

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبة - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji027-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

Alhidaaya.com

Adabu Za Kula

027-Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula

12-  Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula.  Kati ya du’aa zilizothibiti kwa hilo ni:  

"أَفْطَـرَ عِنْدَكُمُ الصَّـائِمُوْنَ ، وَأَكَلَ طَعَامَـكُمُ الأبْـرَارُ ، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُ الملائِكَـةُ"

“Wamefungua kwenu waliofunga, na wamekula chakula chenu watu wema, na Malaika wamewaombeeni rahmah”.   [Hadiyth Swahiyh kwa wenza wake.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3854), Ibn Maajah (1747) na wengineo].

 "اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ"

“Ee Allaah!  Wabarikie katika Ulivyowaruzuku, Waghufirie na Warehemu”.

[Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (3805), At-Tirmidhiy (3500) na Abu Daawuwd (3241)].