028-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kunong'onezana Wawili Pasina wa Tatu Bila Idhini yake Isipokuwa kwa Haja (Dharura)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن تناجي اثنين دون الثالث بغير إذنه

إِلاَّ لحاجةٍ وَهُوَ أن يتحدثا سراً بحيث لا يسمعهما وفي معناه مَا إِذَا تحدثا

بلسان لا يفهمه

028-Mlango Wa Kukatazwa Kunong'onezana Wawili Pasina wa Tatu Bila Idhini yake Isipokuwa kwa Haja (Dharura)

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ ﴿١٠﴾

Hakika mnong’ono unatokana na shaytwaan [Al-Mujaadalah: 10]

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إِذَا كانُوا ثَلاثَةً ، فَلاَ يَتَنَاجَى اثْنَانِ دُونَ الثَّالِثِ )) . متفق عَلَيْهِ .

ورواه أَبُو داود وزاد : قَالَ أَبُو صالح : قُلْتُ لابنِ عُمرَ : فَأرْبَعَةً ؟ قَالَ : لا يَضُرُّكَ .

ورواه مالك في "الموطأ" : عن عبد الله بن دينارٍ ، قَالَ : كُنْتُ أنَا وابْنُ عُمَرَ عِنْدَ دَارِ خَالِدِ بنُ عُقْبَةَ الَّتي في السُّوقِ ، فَجَاءَ رَجُلٌ يُريدُ أنْ يُنَاجِيَهُ ، وَلَيْسَ مَعَ ابْنِ عُمَرَ أَحَدٌ غَيْرِي ، فَدَعَا ابْنُ عُمَرَ رَجُلاً آخَرَ حَتَّى كُنَّا أَرْبَعَةً ، فَقَالَ لِي وَللرَّجُلِ الثَّالِثِ الَّذِي دَعَا : اسْتَأْخِرَا شَيْئاً ، فَإنِّي سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقُولُ : (( لا يَتَنَاجَى اثْنَانِ دُونَ وَاحِدٍ )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mkiwa watu wa tatu (katika kikao), wawili kati yao wasinong'onezane bila ya yule wa tatu." [Al-Bukhaary, Muslim, Abu Daawuwd na Maalik].

Na amepokea Abu Daawuwd na akaongeza: Amesema Abu Swaalih: "Nilimuuliza Ibn 'Umar: Je wakiwa watu wane?" Akasema: "Katika hali hiyo hatakuwa na madhara yoyote (hapa tatizo)."

Na amepokea Maalik katika Al-Muwatwa kwamba 'Abdillaah bin Dinaar amesema: "Nilikuwa pamoja na Ibn 'Umar ndani ya nyumba ya Khaalid bin 'Uqbah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alikuwa sokoni. Alikuja mtu ambaye alitaka kumnong'oneza na hakukuwa na mtu mwengine isipokuwa mimi. Ibn 'Umar alimuita mtu mwengine na hivyo tukawa watu wane. Hapo akaniambia mimi na yule mtu wa tatu aliyemuita, jiongeeni kidogo kwani nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Hawanong'onezani watu wawili na kumuacha mmoja kando." 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعود رضي الله عنه : أنَّ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إِذَا كُنْتُمْ ثَلاَثَةً ، فَلاَ يَتَنَاجَى اثْنَانِ دُونَ الآخَرِ حَتَّى تَخْتَلِطُوا بِالنَّاسِ ، مِنْ أجْلِ أنَّ ذَلِكَ يُحْزِنُهُ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Munapokuwa watu watatu, wasinong'onezane watu wawili pasina yule watatu mapak mchanganyikane na watu wengine, kwani jambo hilo litamhuzunisha sana." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Share