01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Udhwhiyah: Taarifu Yake Na Uhalali Wake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

الأُضْحِيَةُ

 

 Udhwhiyah  

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

01-Udhwhiyah: Taarifu Yake Na Uhalali Wake:

 

 

"الأُضْحِيَةُ" , kwa kutia dhwamma juu ya alif (al-udhwhiyah), pia inafaa kutia kasrah ( "الأِضْحِيَةُ"al-idhwhiyah), na pia inajuzu kuondosha hamzah na kufatihisha dhwaad  "ضَحِيَةٌ") dhwahiyatun), ni mnyama anayechinjwa kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah Ta’aalaa katika yale Masiku ya kuchinja kwa masharti maalum.  Ni kama vile amenyambulika kutokana na jina la wakati ambao imewekwa sharia ya kumchinja ndanimwe, na kwa hivyo akaitwa kwayo Yawm Al-Adhwhaa (Siku ya kuchinja).  [Subulus Salaam (4/160) na Ibn ‘Aabidiyna (5/111].

                        

 

Uhalali Na Usharia Wake:

 

Asili ya uhalali wa udhwhiyah ni Qur-aan, Sunnah na Ijmaa.  Ama katika Qur-aan, ni Kauli Yake Ta’aalaa:

 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

 

2.  Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja.  [Al-Kawthar : 02].

 

Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kuwa muradi wa Aayah hii ni kuchinja udhwhiyah baada ya Swalaatul ‘Iyd. 

 

Ama Sunnah, Anas amesema:  

 

"ضَحَّى النَّبِيُ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ ‏، وَسَمَّى وَكَبَّرَ ، وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا"

 

“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja beberu wawili wenye rangi mseto ya weupe na weusi na wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akapiga Bismil Laahi, akaleta Takbiyr, na akaweka mguu wake juu ya bapa za shingo zao”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5558) na Muslim (1966)].

 

Na Waislamu wote wanajua uhalali wa udhwhiyah.  [Al-Mughniy (9/345), Al-Haawiy cha Al-Mawruwdiy (19/83) na Al-Muhallaa (7/355)].

                                                                         

 

Share