046-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karaha ya Kutembea na Kiatu Kimoja au Soksi Moja Bila Udhuru Wowote na Karaha ya Kuvaa Viatu au Soksi kwa Kusimama Bila Udhuru

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة المشي في نعل واحدة أو خف واحد

لغير عذر وكراهة لبس النعل والخف قائماً لغير عذر

046-Mlango Wa Karaha ya Kutembea na Kiatu Kimoja au Soksi Moja Bila Udhuru Wowote na Karaha ya Kuvaa Viatu au Soksi kwa Kusimama Bila Udhuru

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَيَمشِ أحَدُكُمْ فِي نَعْلٍ وَاحِدَةٍ ، لِيَنْعَلْهُمَا جَمِيعاً ، أو لِيَخْلَعْهُمَا جَمِيعاً )) .

وفي رواية : (( أو لِيُحْفِهِمَا جَمِيعاً )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asitembee mmoja wenu na kiatu kimoja, na avae vyote au avue vyote." 

Na katika riwaayah nyengine: "Au aiache miguu yote mitupu (atembee bila viatu)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : سمعت رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إذا انْقَطَعَ شِسْعُ نَعْلِ أَحَدِكمْ ، فَلاَ يَمْشِ في الأُخْرَى حَتَّى يُصْلِحَهَا )) . رواهُ مسلم .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Unapokatika ukanda mmoja wa kiatu cha mmoja wenu, asitembee na kile kiatu chengine mpaka akitengeneze (akirekebihse)." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم نَهَى أنْ يَنْتَعِلَ الرَّجُلُ قَائِماً . رواه أبو داود بإسناد حسن .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemkataza mtu kuvaa viatu akiwa amesimama." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]

 

Share