01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: (Vinywaji) Taarifu Yake Na Asili Ya Uhalali Wake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

الأَشْرِبَةُ

 

Vinywaji 

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

01- Vinywaji: Taarifu Yake  Na Asili Ya Uhalali Wake:

 

 

Vinywaji "الأَشْرِبَةُ" , ni wingi wa "شَرَابُ" kinywaji, na "الشَّرَابُ"  ni jina la chochote kinachonywewa kwa aina yake yoyote kiwavyo, ni sawa yawe maji au kinginecho, na kwa hali yoyote kiwavyo, na kila kitu kisichotafunwa, basi husemwa kuwa kinanywewa.  [Lisaanul ‘Arab na Mukhtaar As-Swihaah].

 

·        Asili Ya Vinywaji Vyote Ni Halali Ila Vile Vilivyoharamishwa Na Qur-aan Au Hadiyth:

 

Ni kwa ujumuishi wa dalili zilizotajwa kwenye mlango wa vyakula nyuma zinazothibitisha uasili wa uhalali, lakini pia kwa Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu):

 

" لَقَدْ سَقَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِهَذَا الْقَدَحِ الشَّرَابَ كُلَّهُ، الْمَاءَ، وَالنَّبِيذَ، وَالْعَسَلَ، وَاللَّبَنَ‏"

 

“Kwa hakika nilimnywesha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vinywaji vyote kwa kikombe hiki; maji, juisi ya zabibu, asali, na maziwa”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2008) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (1/294)].

 

 

 

 

Share