10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Kwanza

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

10-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram):  Kauli Ya Kwanza:

 

‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu idadi ya manyonyesho ya kufikisha kwenye uharamu ambayo yanathibiti kwayo hukmu ya kunyonya katika kauli nne:

 

Ya kwanza: 

 

Nyonyesho moja na zaidi linaharamisha.  Ni kauli ya Jumhuwr, Ibn Al-Musayyib, Al-Hasan, Az-Zuhriy, Qataadah, Al-Awzaaiy, Ath-Thawriy na Al-Layth.  Dalili zao ni:

 

1-  Ujumuishi wa Kauli Yake Ta’aalaa:  

 

"وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ"

 

“Na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya”.  [An-Nisaa: 23]

 

2-  Ujumuishi wa kauli ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"إِنَّما الرَّضَاعَةُ مِنَ المَجَاعَةِ"

 

“Nyonyesho kamili ni lile la (kumshibisha) mtoto mwenye njaa”.  [Al-Bukhaariy (5102) na Muslim (1455)]

 

3-  Neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"يَحْرُمُ مِنَ اَلرَّضَاعِ مَا يَحْرُمُ مِنْ اَلنَّسَبِ"

 

Lililo haramu kwa sababu ya kunyonya ni haramu pia kwa sababu ya nasaba”. [Hadiyth Swahiyh.  Imetajwa nyuma]

 

4-  Hadiyth ya ‘Uqbah bin Al-Haarith aliyesema:

 

"تَزَوَّجْتُ امْرَأَةً فَجَاءَتْنَا امْرَأَةٌ سَوْدَاءُ فَقَالَتْ إِنِّي قَدْ أَرْضَعْتُكُمَا‏.‏ فَأَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرْتُهُ فَقُلْتُ: إِنِّي تَزَوَّجْتُ فُلاَنَةَ بِنْتَ فُلاَنٍ فَجَاءَتْنِي امْرَأَةٌ سَوْدَاءُ فَقَالَتْ: إِنِّي قَدْ أَرْضَعْتُكُمَا‏.‏ فَأَعْرَضَ عَنِّي فَأَتَيْتُهُ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ فَقُلْتُ: إِنَّهَا كَاذِبَةٌ.‏ قَالَ:‏ وَكَيْفَ بِهَا وَقَدْ زَعَمَتْ أَنَّهَا قَدْ أَرْضَعَتْكُمَا دَعْهَا عَنْكَ"

 

“Nilioa mwanamke kisha akatujia mwanamke mmoja mweusi akatuambia: Nimekunyonyesheni.  Nikamwendea Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikamwambia:  Nimemwoa fulani binti fulani, halafu akatujia mwanamke mweusi akaniambia:  Mimi nimewanyonyesheni, naye ni mwongo.  Rasuli akanipa mgongo nami nikamjia mbele ya uso wake nikamwambia:  Hakika yeye ni mwongo.  Akasema:  Wewe vipi unamuingilia mkewe na huyo mwanamke amedai kwamba amewanyonyesheni!  Mwache mkeo”.  [Al-Bukhaariy (2659), At-Tirmidhiy (1151) na An-Nasaaiy (3330)]

 

Wamesema kwamba Aayaat na Hadiyth hizi na nyinginezo hazikutaja idadi maalum.

 

5-  Wamezijibu riwaayah ambazo zimeainisha idadi ya manyonyesho yenye kuharamisha (ambayo yatakuja elezewa mbeleni) kwamba idadi yake imetofautiana na ile iliyotajwa na ‘Aaishah, hivyo ni wajibu kurejea kwenye idadi ndogo zaidi iliyotajwa.

 

6-  Toka kwa ‘Amru bin Diynaar amesema: 

 

"أَتُحَرِّمُ رَضْعَةُ أَوْ رَضْعَتَانِ؟ فَقَالَ: مَا نَعْلَمُ الأُخْتَ من الرَّضَاعَةِ إِلا حَرَامًا، فَقَالَ رَجُلُ: إِنَّ أَمِيْرَ المُؤْمِنِيْنَ -يُرِيْدُ ابن الزُّبَيْرِ- يَزْعُمُ أَنَّهُ لا تُحَرِّمُ رَضْعَةٌ ولا رَضْعَتَانِ"

 

Nilimsikia Ibn ‘Umar alipoulizwa swali na mtu lisemalo:  Je, nyonyesho moja linaharamisha au mawili?  Akajibu:  Hatumtambui dada wa kunyonya kwa jingine isipokuwa ni haramu kuolewa.  Mtu yule akasema:  Amiri wa Waumini -yaani Ibn Az-Zubayr- anadai kwamba nyonyesho moja au mawili hayaharamishi.  Ibn ‘Umar akamwambia:  Hukmu ya Allaah ni bora zaidi kuliko hukmu yako na hukmu ya Amiri wa Waumini”.   [Isnadi yake ni Swahiyh.  Imekharijiwa na Abdulrazzaaq (7/467) na Al-Bayhaqiy (7/458)]

 

7-  Kwa vile kitendo hiki kinahusiana na uharamu wa milele, idadi haijazingatiwa kama ulivyo uharamu wa mama za wake.

 

 

Share