11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Pili

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

11-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram):  Kauli Ya Pili:

 

Manyonyesho matatu na zaidi yanaharamisha.  Ni riwaayah ya tatu toka kwa Ahmad, kauli ya Ahlu Adh-Dhwaahir, Is-haaq, Abu ‘Ubayd, Abu Thawr na Ibn Al-Mundhir.  Dalili zao ni:

 

1-  Hadiyth ya ‘Aaishah:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"لا تُحَرِّمُ اَلْمَصَّةُ وَالْمَصَّتَانِ"

 

“Kunyonya mtoto mara moja au mara mbili hakuharamishi”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1450), Abu Daawuwd (2063), At-Tirmidhiy (1150), An-Nasaaiy (6/101) na Ibn Maajah (1941)]    

 

2-  Hadiyth ya Ummul Fadhwl amesema: 

 

"دَخَلَ أَعْرَابِيٌّ عَلَى نَبِيِّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ فِي بَيْتِي فَقَالَ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي كَانَتْ لِي امْرَأَةٌ فَتَزَوَّجْتُ عَلَيْهَا أُخْرَى فَزَعَمَتِ امْرَأَتِي الأُولَى أَنَّهَا أَرْضَعَتِ امْرَأَتِي الْحُدْثَى رَضْعَةً أَوْ رَضْعَتَيْنِ.‏ فَقَالَ نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:‏ لاَ تُحَرِّمُ الإِمْلاَجَةُ وَالإِمْلاَجَتَانِ‏"

 

“Bedui alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye yuko nyumbani kwangu akasema:  Ee Nabiy wa Allaah!  Nilikuwa na mke halafu nikamwolelea mke mwenza.  Mke wangu mkubwa akadai kwamba amemnyonyesha mke huyo mdogo nyonyesho moja au mawili.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  Nyonyesho moja au mawili hayaharamishi”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1451), Ahmad (6/339) na Al-Bayhaqiy (7/455)]

 

 

Share