17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Walioharamika Kwa Muda: ii-Khalati Ya Mke Au Shangazi Yake:

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

17- Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 2-Khalati Ya Mke Au Shangazi Yake:

 

Abu Hurayrah:   “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"لَا يُجْمَعُ بَيْنَ الْمَرْأَة وعَمَّتِهَا وَلَا بَينَ الْمَرْأَة وخَالَتِهَا"

 

“Mwanamke haolewi ndoa moja na shangazi yake wala na khalati yake”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5109) na Muslim (1408)]

 

Jaabir kasema:

 

"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تُنْكَحَ الْمَرْأَةُ عَلَى عَمَّتِهَا أَوْ خَالَتِهَا‏"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza shangazi au khalati kuwa mke mwenza wa mwanamke.”  [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5108) na An-Nasaaiy (6/98)]

 

Kwa muktadha huu, kwa mujibu wa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa, si halali mtu kumkusanya mwanamke na shangazi yake au khalati yake ndani ya ndoa moja, ni sawa awe shangazi au khalati wa kweli au wa kimajazi.  Wa kimajazi ni dada wa baba wa baba, na baba wa babu na kwenda juu.  Au dada wa mama wa mama (bibi), na mama wa bibi kwa upande wa mama na kwa upande wa baba na kwenda juu.  Hawa wote ni haramu kuwakusanya ndani ya ndoa moja.

 

 

Share