07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Mavazi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

06:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  3-Mavazi:  

 

‘Ulamaa kwa itifaki moja wamekubaliana kwamba ni wajibu kwa mume kumnunulia mavazi mkewe kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada”.  [Al-Baqarah: 233]

 

Na Hadiyth ya Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu):

 

"اتَّقوا اللهَ في النِّسَاءِ، فإنَّهُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ، أَخَذْتُمُوْهُنَّ بِأمَانةِ اللهِ، وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوْجَهُنَّ بِكَلِمَةِ اللهِ َوَلَهُنَّ عَلَيْكُمْ رِزْقُهُنَّ وكِسْوَتُهنَّ بِالمعْرُوْفِ"

 

“Mcheni Allaah katika kuamiliana na wanawake, kwani wao ni mateka walio mikononi mwenu, mmewachukua kwa Dhamana ya Allaah, mmehalalikiwa tupu zao kwa Neno la Allaah, nanyi ni wajibu wenu kuwalisha na kuwavisha kwa mujibu wa ada”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (1218)]

 

Mavazi ni jambo la kudumu, na kwa hivyo, ni lazima mume ampatie mkewe mavazi ya kutosha kuanzia mavazi ya ndani, ya kutokea, na ya minasaba kwa mujibu wa hali, na kwa mujibu wa urefu wake, ufupi wake, unene wake, wembamba wake na kadhalika.  Pia, yaendane na mazingira ya nchi waliyopo kama ni ya joto au baridi na kadhalika.

 

 

Share